Redcross(TRCD),imetoa msaada wa fedha kwa kaya 500 katika wilala ya Mburu na Simanjiro
Na Yasmine Protace
TANZANIA Redcross(TRCD),imetoa msaada wa fedha kwa kaya 500 katika wilala ya Mburu na Simanjiro,ambapo Wilaya hizo zimeathiliwa na ukame.
Msaada huo ulikabidhiwa na Katibu mkuu wa Tanzania Redcross Sociéy , Felician Mtahengerwa ambaye aliambatana na mwenyekiti wa Redcross wakili Moses Basila. .
Katika kugawa msaada huo pia mkurugenzi wa Maendeleo ya Taasisi na Miradi Reginald Mhango ameungana na wafanyakazi wa TRCS na IFRC katika zoezi la kugawa msaada wa kifedha kwa kaya 500.
"Kaya zilizo athirika na ukame ni 200 katika wilayani simanjiro,Mkaoni Manyara ,"alisema.
Aliongeza kuwa kaya hizo 200 zimenufaika na msaada huo wa TRCS chini ya ufadhili wa IFRC.
Katika msaada huo, Katibu wa RedCross amekutana na mkuu wa wilya ya simanjiro Suleiman Serera ambaye ameipongeza Red Cross kwa kazi zake nakusema anawakaribisha muda wowote kwa ushirikianoSerera ameiomba TRCS kuangalia uwezekano wakusaidia Wilaya hiyo program za kutokomeza ukame .
Kwa mujibu wa Katibu wa TRCD zoezi la kugawa msaada zoezi lilianza Aprili 27 mwaka huu wilayani Mburu amabapo kaya 100 zilinufaika na hivyo kuleta jumla ya kaya 300 mkoani humo.
Kwa mujibu wa Katibu huyo pia kaya 200 za Mburu Mkoani Arusha zilinufaika na zoezi hilo.


No comments
Post a Comment