Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango kuzindua Kongamano la 31 la kisayansi la NIMR
Na Mussa Agustine.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la 31 la Kisayansi la Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) linalofanyika Mei 17 mwaka huu.
| Mkurugenzi Mkuu wa NIMRI Profesa Yunus Mgaya |
"Nafurahi kieleza kwamba mafanikio makubwa yaliyotokana na kuratibu makongamano haya,yameleta chachu ya mwendelezo na mwaka huu (2022) tunaratibu kongamano la 31,ni kongamano la siku tatu linatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 17 /05/2022 na Makamu wa rais Daktari.Philip Mpango katika kituo Cha Kimataifa Cha Julius Nyerere Dar see salaam" amesema Profesa Mgaya.
Ameendelea kufafanua kwamba kupitia kongamano hilo inasaidia kuibua na kubainisha maeneo muhimu ya afya yanayohitaji hatua za haraka za kitafiti zitakazoleta mabadiliko ya sera ,miongozo,mifumo ya tiba na utendaji Kwa lengo la kuboresha afya ya jamii.
"Tuanapozungumzia huduma ya afya Kwa Wote tunamaanisha wananchi wote waweze kufikiwa na huduma muhimu za Afya zinazohusisha uelimishaji kuhusu afya bora,Kinga,matibabu,utunzaji wa dawa na hatimaye uboreshwaji wa maisha ya Mtanzania Kwa ujumla,kongamano hili linashirikisha watalaam zaidi ya miatatu kutoka katika taasisi mbalimbali za Kitaifa nchini Tanzania naza kimataifa wakiwemo watafiti na watunga sera" amesisitiza Mkurugenzi hiyo wa NIMR.
Hata hivyo ameongeza kwamba maandiko 260 yakisayansi yanatarajiwa kuwasilishwa katika kongamano hilo kupitia mada ndogondogo zitakazohisu Magonjwa mbalimbali ,vichocheo vyake na ufanisi katika mfumo wa afya kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo Magonjwa ambukizi,Tiba asili,Usugu wa dawa katika tiba ya Magonjwa na mifumo ya udhibiti wa Magonjwa.
Maeneo mengine ni Afya ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi, Magonjwa yasiyoambukiza,huku eneo jingine ni Changamoto za Afya zitokanazo na janga la UVIKO 19 ,Lishe,Afya ya mama,mtoto na Vijana,Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele,pamoja na udhibiti na usimamizi wa tafiti za Tiba.
| Mkurugenzi Mratibu wa Taarifa na Mawasiliano ya Kitafiti NIMR, Dr. Ndekya Oriyo. |
Kwa upande wake Mkurugenzi Mratibu wa Taarifa na Mawasiliano ya Kitafiti Dr Ndekya Oriyo amesema kwamba Nchi mbalimbali zimethibitisha kushiriki kwenye kongamano hilo ikiwemo Marekani,Ujerumani,Uganda, Uingereza,Senegari,Afrika Kusini,ambapo litasaidia kujadili Kwa pamoja changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya afya.
No comments
Post a Comment