ACT Wazalendo yaishauri Serikali Kuhusu Uboreshaji wa Elimu.
Na Mussa Augustine.
Chama Cha Act Wazalendo kimesema kwamba Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia inatakiwa kuwa na Usimamizi na Umakini mzuri wa kupanga Bejeti inayojitoshereza ya Wizara hiyo ili itoshereze katika kuboresha mfumo Mzuri wa Elimu kwa wanafunzi.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Sekta ya Elimu wa Chama hicho Riziki Shahari Mngwali wakati akizungumza na waandishi was habari kuhusu bajeti ya Wizara ya Elimu iliyopitishwa hivi karibuni Bungeni Jijini Dodoma,ambapo amesema kuwa bajeti za Wizara hiyo zimekuwa zikipitishwa lakini hazileti mabadiliko yoyote katika Sekta ya Elimu.
Aidha amesema kwamba kumekuwa na kasumba ya kila Waziri anaeteuliwa katika nafasi hiyo anakuja na mipango yake,hivyo kuifanya Sekta ya Elimu kulegalega kutokana na kukosekana kwa miundombinu Bora itakayowafanya wanafunzi kupata Elimu Bora.
" Kila Waziri anaeteuliwa anakuja na lake ,Mara tubadilishe Mitaala,Mara wanafunzi wasifundishwe twisheni,hali hiyo ni taharuki kwenye Sekta ya Elimu, Sisi Kama Act Wazalendo tunaishauri Serikali itimize wajibu wake, hotuba ya bajeti iliyotolewa ya mwaka wa fedha 2022/ 23 haina majibu ya changamoto au mapungufu ya Elimu yanayopigiwa kelele na vyama vya upinzani lakini hayafanyiwi kazi" amesema Bi.Riziki.
Nakuongeza kwamba "Kinachotakiwa kwa sasa Waziri mwenye dhamana ya Elimu aanzishe Baraza au Bodi ya Ushauri wa Elimu ili kumshauri Wzairi nini kifanyike ili mfumo wa Elimu uwe Bora na kuweza kutoa elimu Bora kwa wahitimu.
Hata hivyo amesema kwamba Mfumo wa Elimu ya sekondari unakumbwa na changamoto mbalimbali licha ya Elimu hiyo kutolewa bure ikiwemo Upungufu wa Walimu wenye sifa, Upungufu wa vyumba vya madarasa na Vitabu hali ambayo chama hicho kimeshauri changamoto hizo zitafutiwe ufumbuzi kwa kutenga bajeti ya Wizara ya Elimu inayojitoshereza.
No comments
Post a Comment