Zinazobamba

Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imezipiga faini kampuni nne za Bima.

Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imezipiga faini kampuni nne za Bima kwa kukiuka kanuni namba 10 ya Sheria ya Bima ya mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake.

Akizitaja kampuni hizo ni pamoja na kampuni ya UAP, Jublee Insurance, Insurance Group of Tanzania (IGT) huku kampuni ya Resolution Insurance ikiwekewa zuio la kutoendelea kuandikisha  na kuchukua biashara yoyote mpya kuanzia sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamishna wa TIRA Dr Baghayo Saqware amesema Soko la Bima la Tanzania licha ya kuwepo kwa changamoto ndogo ndogo lanaendelea kukua kwa asilimia 10, hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi kwani mamlaka hiyo inafanya kazi zake kwa umakini.

Akizitaja kampuni hizo ni pamoja na kampuni ya Bima ya Insurance Group of Tanzania (IGT) ambayo imepigwa faini ya shiling milioni 20 ambapo Mwenyekiti wa bodi ya kampuni hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu, Afisa fedha Mkuu pamoja na Meneja wa madai na fidia wakitakiwa kulipa kila mmoja shilingi milioni tano.

Amesema kuwa, hatua hiyo imekuja kwa kuzingatia kifungu namba 166(1) cha sheria ya Bima nchini ambayo pia imeiagiza kampuni hiyo kulipa wadai wote wapatao 48 ambao imeshawapatia hati ya kukubali madai ndani ya siku 14.

Pia ameitoza faini kampuni ya Jubilee shilingi  milioni 5 ambayo tayari  imeshalipwa huku ikiamuru kampuni hiyo kulipa fidia ya kiasi Cha Euro milioni 511 kama inavyodaiwa na Wizara ya Maji baada ya kampuni ya ukandarasi ya Spencon kushindwa kutimiza wajibu wake wa kimkataba wa miradi ya maji wenye mkataba namba ME-011/2011-2012/W/O5 kwa Mamlaka ya maji ya mji wa kigoma ambao ulikua umepewa Kinga na kampuni ya Jubilee.

Hata hivyo, pia Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jubilee ametozwa faini ya shilingi milioni 10 kwa kutofuata taratibu za kibima hivyo, kupelekea kuchafua taswira ya Soko la bima nchini.

Akitaja kampuni nyingine ya Bima ni UAP ambapo amesema kwa nyakati tofauti kuanzia tarehe 01/10/2021-06/05/2022 imepokea malalamiko  zaidi ya manne kuhusu kampuni   kampuni hiyo.

Aidha mamlaka ya usimamizi wa  Bima Nchini  (TIRA) inapenda kuwajulisha watanzania kuwa kampuni zote za bima nchini zitatakiwa kuleta taarifa za madai yote yaliyowasilishwa kwa watu za kiutendaji au usuluhusho walizofikia kila robo ya mwaka .

No comments