Zinazobamba

Serikali na wadau wa Elimu watakiwa kuwekeza nguvu katika elimu ya Kidijitali ili watoto waendane na Dunia ya leo

Umoja wa Mameneja na Wamiliki wa shule na vyuo visivyo vya serikali (TAMONGSCO) Umeiomba serikali Pamoja na wataalamu mbalimbali wa elimu kushirikiana, ili kuwawezesha Watoto kuweza kuyatumia vizuri mabadiliko ya kudijital kwa kuyageuza mabadiliko hayo kuwa uwanja mzuri wa kujifunzia na kupanua uwanja wa watoto kujisomea ili kusiwepo na mtoto anayeachwa nyuma.

Hayo yameelezwa mapema Mei 8, 2022 na Alfred Luvanda ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Mameneja na Wamiliki wa Shule na Vyuo visivyo vya Serikali (TAMONGSCO) wakati akiendesha mashindano ya Chemsha Bongo baina ya shule 10 za jijini Dar es salaam.

Aidha Mwenyekiti huyo amesema kuwa hii ni kama sehemu ya kuendeleza utamaduni wa kujisomea na kujiendeleza katika elimu kuwa uwepo wa Majukwaa ya Kidijital yenye kutoa fursa kwa Watoto kuweza kujisomea masomo mbalimbali shuleni kwa njia ya dijital ikiwemo Jukwaa la TESEA.

Ameongeza kuwa ni hatua muhimu ya kuweza kuungana na wengine kuwasilisha suluhu zinazounganishwa na Teknolojia ili kusiwe na mtoto atakaye achwa nyuma, kwa kuhakikisha kila mwanafunzi anapata nyenzo za kujifunzia kupitia majukwaa ya kidijitali sanjari na mataifa mengine duniani ili kufanya taifa kunufaika na maendeleo hayo ya Teknolojia.

Baadhi ya wanafunzi waliyoshiriki katika mashindano hayo ya Chemsha Bongo.

Aidha kwa upande wa Mkurugenzi wa Dijital Academia Limited (DATL) Mombo Kaleo amesema muda wa sasa kwenye elimu ni kwenye Dijitali kwani hiyo ni njia pekee inayoweza kumuhakikishia kila mwanafunzi wa kitanzania kupata nyenzo zote za kujifunzia kwenye ncha za mikono yake.

Ameendelea kusema kuwa si nyenzo tu bali ni nyenzo zilizo sawa na mtaala wa taifa na kuwafanya Watoto kuwa na matumizi mazuri ya mabadiliko ya Dijitali.

Shughuli ikiendelea.

No comments