Zinazobamba

Kongamano la Uzinduzi wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu J.K Nyerere Kufanyika Mei 14, Jijini Dodoma

Leo Mei 8, 2022 jijini Dar es salaam.

Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwl.J.K. Nyerere inayoongozwa na Mwenyekiti wake Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Mizengo Pinda imekutana hii leo Jijini Dar es salaam kwa kikao chake Cha kawaida kwa ajili ya kuzungumzia Kongamano na Uzinduzi wa taasisi hiyo utakaofanyika Mei 14 Mwaka huu jijini Dodoma.

Akiongoza kikao hicho Makamu Mwenyekiti wa bodi hiyo  Waziri Mstaafu Mh. Zakhia Meghji amesema kwamba Wajumbe wa Bodi ya Sekretarieti ya Taasisi hiyo watashiriki katika tukio muhimu la kitaifa.

Aidha Makamu  Mwenyekiti huyo amewataka wajumbe hao washirikiane kwa pamoja katika kufanikisha maandalizi ya kufanyika kwa  kongamano na Uzinduzi wa Taasisi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Taifa Waziri Mstaafu Mh.Paul Petro Kimiti amewashauri wajumbe wa Sekretarieti hiyo kuhakikisha wanatekeleza maagizo ya Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi hiyo ili kuweza kufanikisha Uzinduzi wa Taasisi  Jijini Dodoma utakaofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Conversion Centre ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Majaliwa Kassim Majaliwa. 

Katika kikao hicho pia kimehudhuliwa na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi hiyo anayehusika na uhusiano  wa mambo ya nje Waziri Mstaafu Mh. Prof. Anna Tibaijuka pamoja na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi hiyo Waziri Mstaafu Dkt.Maua Daftari. 

 Moshi said
Afisa habari wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwl.J.K.Nyerere.

No comments