Mwamko sekta ya Islamic Banking wazidi kuimarika, NBC warudi kwa kishindo
Meneja mahusiano wa Benki ya maendeleo ya NBC Tanzania Bw Ally Abdul amewaomba Waislam na wasio waislam kuipokea benki hiyo kwa mikono miwili kwenye huduma ya Islamic Banking kwani sasa wameamua kurudi kwa nguvu kubwa kuhudumia jamii ambayo kiasili hawapendi kutumia benki ambazo zinatoza riba.
Akizungumza na Waislam Mei 6, 2022 kwenye swala ya Ijumaa iliyofanyika katika msikiti wa Mtambani Jiji Dar es Salaam, Abdul alisema benki imedhamiria kutoa huduma bora kwenye sekta hiyo.
“NBC ndio waanzilishi wa huduma
za kifedha kwa mfumo wa Kiislam Tanzania, ilianza Mei 5, 2010, lakini kutokana
na sababu zisizo zuilika ikawa haikuwa kwenye matangazo mengi, ndio maana ikawa
kama iko chini, ispokuwa kwa sasa NBC tumerudi, tena tumerudi kwa nguvu kubwa,
tutatumia mifumo yetu ambayo imeenea kila sehemu Tanzania kutangaza Islamic
Banking,” alisema
Aidha, Mtaalam huo wa masuala ya
mahusiano ya umma alisema benki yao imejipanga vizuri kuhakikisha huduma
wanazotoa zinafuata sheria zote zinazoongoza sekta hiyo na tayari wanayo bodi
yenye weledi mkubwa wa kushughulika na masuala hayo.
Pia alisema kwa sasa benki ya NBC
wanabidhaa aina mbili, mosi ni akaunti za akiba lakini bidhaa ya pili ni
biashara ya mikopo.
“Kwenye upande wa kuwekeza tunayo
La riba saving akaunti, la Riba business akaunti na Privilege akaunti kwa ajili
ya watu wanaohitaji huduma yenye upekee hasa wafanya biashara,
Vilevile, ipo akaunt ya La riba
Fixed Akaunti, ambayo upekee wake mkubwa ni kwamba inayo uwezo wa kuenda mpaka
miaka 5, “Yaani mteja anaweza kuwa na fedha yake mfano laki 5 au million 5, 10,
100 basi anaweza kuja kuiweka benki kwa muda anaotaka, ikumbukwe wakati fedha
yake ikiwa benki itafanyiwa biashara na atapata gawio,” alisema
Aidha, akifafanua gawio
linavyopatikana, Abdul alisema fedha inayowekwa katika akaunti ya Fixed
inakopeshwa kwa wateja kwa kufuata misingi ya uislam na faida inayopatikana
inagawanya pande mbili, benki na mmiliki wa fedha.
“Namna ya kuchukua gawio husubil
mpaka miaka mitano iishe, faida yake inaweza kuchukua muda wowote, kuanzia
miezi mitatu, miezi sita, mwaka na kadharika,”alisema
La Riba Busines akaunti ni kwa
ajili ya wafanyabishara, unakuta mtu ana fedha nyingi hataki zikae nyumbani,
anataka kuweka benki ili achukue kwa kuendesha biashara yake.
Mbali na biashara hiyo ya
kuwekeza fedha benki, pia NBC inafanya biashara ya mikopo isiyo na riba maarufu
kama murabaha.
“Tunatoa mikopo kwa ajili ya
wafanyakazi chini ya uaratibu wa murabaha, lakini pia tunatoa mikopo ya
biashara pamoja, katika biashara hii haihusishi fedha kabisa, tunafanya hivi
ili kuepuka riba,” alisisitiza Bw. Abdul
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) ni
moja ya benki kubwa hapa nchini ambayo inatoa huduma zinazo sifiwa.
No comments
Post a Comment