Mkurugenzi Kituo cha Kimisri aaga Waislam Mtoro, aacha wosia mkubwa
Ni miaka mitatu sasa toka Mudiri wa Markaz Chang’ombe Sheikh Abdul-Mu’ty afike nchini kuendeleza mafundisho sahihi ya uislam kwa Taifa la Tanzania. Hivi
sasa kiongozi huyo anayetibu nyoyo muda wake wa kuishi nchini umekwisha na anatarajia kurejea nchini kwake Misri hapo Mei 8, 2022. Gazeti imaani limebahatika kufanya mahojianao naye likitaka kujua baadhi ya mambo kadhaa, ungana na Suleiman Magali kuelewa kwa kina zawadi aliyowaachia watanzania
Mwandishi wetu: Wewe kiongozi mkubwa wa Markazi hii na unaondoka
mei 8, 2022 baada ya kukamilika muda wako, pengine upi ushauli wako kwa waislam
wa Tanzania
Sheikh Abdul-Mu’ty: Yapo mengi ya kushauri lakini kubwa
nililoliona ni umuhimu wa Mufti wa Tanzania katika kuenenza dawa, huyu ni mtu
safi sana, niwaombe Viongozi wa Tanzania, Maimamu na Masheikh wajitahidi
kumuunga mkono, wajitahidini sana kuwa nyuma yake kwani ni kiongozi
aliyebalikiwa tabia nzuri ukarimu na usamehevu.
Mwandishi
wetu: Msomaji angependa kujua mambo ambayo hutayasahahu hata ukiwa nchini Misri
katika kipindi chako chote ulichoishi hapa nchini
Sheikh Abdul-Mu’ty: Nikili kuwa sitasahahu ushirikiano mzuri ambao
nimepewa na ofisi ya Bakwata nchini Tanzania na Taasisi zingine. Waislam wa
Tanzania ni watu wakarimu sana na wanao penda dini.
Kipekee nikili kuwa sijawahi kuona kiongozi mwenye sifa nzuri kama
za Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari Zubeir, kiongozi huyu ni
msamehevu, mpenda watu, mpole, mkirimu, anawajali wayonge mafakiri, na
masikini. Nimeishi nchini Misri na kukutana na viongozi Mbalimbali, lakini
mfano wa Mufti Zubeir bado sijapata kuona.
Lakini jambo la pili ambalo sitasahahu hata nikiwa wapi ni
mashindano ya quran. Sijawahi kuona sehemu yeyote mashindano ya quran yanafanyika
kwenye uwanja mkubwa kama wa Mkapa na watu wakafurika vile. Hili jambo limeacha
alama katika nafsi yangu. Sijawahi kuona sehemu yeyote duniani watu wenye
mahaba na quran kama Tanzania.
Mwandishi
wetu: Kitu gani una jivunia katika kipidi chako cha uongozi katika kituo hiki
cha Kimisri
Sheikh Abdul-Mu’ty: Yapo Mengi ya kueleza, lakini kiufupi mimi kwa
kushirikiana na wenzangu tumeweza kuendesha semina mbalimbali za kuelezea kwa
kina fikra sahihi ya uislam. Tumeendesha semina hizo ndani ya kituo lakini pia
nje ya kituo. Hapa niwashukuru sana Bakwata wamekuwa wakitoa ushirikiano mkubwa
kufanikisha shughuli za kidaawa. Hakika naondoka lakini moyo wangu bado upo
Tanzania. Ni sehemu sahihi ya kufanya kazi kwani watu wake ni wakarimu na wenye
upendo wa hali ya juu.
Mwandishi
wetu: Jambo gani limekufurahisha hapa Tanzania?
Sheikh Abdul-Mu’ty: Tanzania ni nchi ya amani na upendo, nimependa watu namna wanavyopendana, kuthaminiana na kujaliana bila kujali dini, rangi.
Licha ya kuwa na dini tofauti lakini siku zote watanzania wamekuwa
wamoja, hilo ni jambo kubwa na ni nadra kuliona katika mataifa mengine.
Kituo cha Markazi Chang’ombe shabaha yake ni kudumisha amani,
nimefurahi zaidi baada ya kuona watanzania wamekuwa mstali wa mbele kudumisha
amani.
Uislam ni amani na sisi shabaha yetu ni kuufundisha uislamu wa
kweli, kuonyesha sura sahihi ya uislamu, kuna watu waliuchafua sana uislamu na
watu wanadhani huo ndio uislamu
Mwandishi
wetu: Jambo gani linakukera na ungetamani litafutiwe ufumbuzi mapema?
Sheikh Abdul-Mu’ty: Jambo ambalo bado linanisikitisha ni
kutokukubalika kwa vyeti vya chuo cha Azhar Sharif hapa Tanzania. Sisi hapa
chuoni tunaona jambo hili haliko sawa, kwa sababu tunaona watoto wetu ni kama
wanabaguliwa, masomo yanayosomwa yangeweza kuwa msaada katika taifa, tunatoa
vijana wazuri waliolelewa kimaadili, wenye kukataa dhulma.
Unakuta mtoto anatumia muda mwingi kusoma, akimaliza masomo yake hapati
kazi serikalini, sababu zakukosa kazi sisi bado hatuelewi.
Vile vile idadi ndogo ya wanafunzi nayo ni jambo ambalo
linatushughulisha, chuo kwa miaka yote imekuwa inatoa huduma zake bure,
inafundisha vijana bila kuwatoza kitu chochote, lakini Chuo kimeenda mbali
Zaidi, sasa hivi kimeongeza idadi ya wanafunzi wanaokwenda kuendelea na masomo
kwa ngazi ya chuo, zamani kilikuwa kinapeleka wanafunzi 4, lakini baada ya
maombi mbalimbali chuo kimekubali kuongeza idadi ya watanzania kwenda kusoma
kutoka wanafunzi 4 hadi kufikia 30, Licha ya uwepo wa nafasi hizo, bado vijana
wameendelea kupungua katika Markazi zetu.
Historia ya
Kituo cha kimisri Tanzania…
Kituo cha Markaz Chang’ombe kilianza mwaka 1965, kilipatikana kama
zawadi iliyotokana na mahusiano mazuri baina ya serikali ya Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania iliyokuwa inaongozwa na Rais wa kwanza wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania na baba wa Taifa hili, Hayati Mwl Jurius Kambarage Nyerere, na Serikali ya Misri.
Kwa pamoja walikubaliana kuja na kitu hiki, kituo kilizinduliwa
rasmi na kufanya kazi zake mwaka 1968,
kilizinduliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mwl. Jurius Nyerere.
Kituo kimeendelea kuwa kitovu cha mahusiano mema baina ya serikali
hizi mbili toka miaka hiyo hadi hivi sasa.
Kupitia kituo cha Kimsri vijana wengi wa kitanzania wamepata elimu
na kujikomboa katika maisha yao, lakini kimekuwa tanuru la kuzalisha walimu
wazuri wa dini ambao wanafundisha uislamu sahihi hapa Tanzania. Vijana wengi wa
Kimisri wamepata fursa ya kuja nchini kufundisha dini,
Mafanikio Makubwa ambayo yamepatikana toka kuanzishwa kwake ni
pamoja na uwepo wa mahusiano mema kati ya kituo na Serikali, kupitia kituo hiki
na mahusiano mazuri yaliyopo Kampuni za nchini Misri zimefanikiwa kupata tenda
ya kujenga Mwalimu Nyerere electric Project ambayo zamani ilikuwa ikifahamika
kama stiglesr George.
Mbali na mahusiano ya kidiplomasia pia kwenye upande wa dini, chuo
kimepata mafanikio makubwa ikiwemo kuweza kufundisha wanafunzi wengi Tanzania
bara na visiwani.
Takribani mikoa na wilaya zote za Tanzania zina wanafunzi kutoka
Markazi, pia katika taasisi nyingi za kidini viongozi wake wakubwa ni mazao
kutoka chuo cha Azhar Shariff. Vilevile kwenye nyumba za ibada nyingi
wanaoongoza swala ni wanafunzi kutoka kituo cha kimisri. Kwa ujumla Kituo cha
Kimisri kimekuwa ni muhimili mkubwa wa kueneza elimu ya dini hapa nchini.
Mazao ya kituo hiki ni pamoja na Sheikh Suleyman Muhammad
Gorogosi, huyu baada ya kurejea kutoka Misri alifanikiwa kushika nafasi kubwa
katika Baraza kuu la waislamu Tanzania (BAKWATA), alifanikiwa kuwa Naibu Mufti
wa Tanzania.
Mwingine ni Sheikh Ali Muhidini Mkoyogole, yeye amefanikiwa kuwa
Naibu Chifu Kadhi Mkuu wa Tanzania.
Wamo pia Sheikh Ali Ngeruko, ambaye ni mjumbe wa Baraza la ulamaa
taifa, Sheikh Shabani Musaa ambaye ni Katiku Mkuu wa Baraza la Sunna Tanzania
(BASUTA), Waziri Amani Maduga wa mkoani Morogoro.
Wengine ni Sheikh Twahir Khaidary Mwinyimvua imaan wa msikiti wa Mwinyikheri, Sheikh Abdallah
Nyumba, Imaam wa msikiti wa Qibratain uliopo Kariakoo, Tanzania na Sheikh Alhad
Musa, ambaye ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Masheikh wa Wilaya wapo Sheikh Zairai Bakari Mkoyogole ambaye ni
Sheikh wa Wilaya ya Temeke, Sheikh Adam Mwinyipingu ambaye anahudumia Wialaya
ya Ilala na Sheikh Mohammad Ahmadi Mulenga anayefanya kazi katika Wilaya ya
Kinondoni.
No comments
Post a Comment