Zinazobamba

RC MAKALA AZINDUA OPARESHENI KABAMBE KUKABILIANA NA PANYAROAD.

Na Mussa Agustino

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Amos Makalla ameagiza kamati ya Ulinzi na Usalama kufanya oparesheni ya kuwasaka vijana maarufu Kama Panyaroad wanaojihusisha na vitendo vya uharifu kwa kujeruhi nakupora vitu mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Amos Makalla
Pia ameagiza kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha inatoa taarifa kila siku za oparesheni ya kupambana na vikundi hivyo vya uhalifu(Panyaroad) ili kusaidia wazazi wa watoto hao kufahamu watoto wao walipo.
Agizo hilo amelitoa Jijini Dar es salaam katika kikao kazi na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo lengo ni kujadiliana mikakati ya kuweza kupambana  na uhalifu wa vijana wanaotembea  mitaani na silaha mbalimbali ikiwemo mapanga nakupora mali mbalimbali ikiwemo Tv ,Simu na  fedha.
Hata hivyo amewataka Wakuu wa Wilaya ,wakuu wa vituo vya polisi wilaya,  kufanya msako kila mahali ili kuwabaini na  kuwakamata wafanya biashara wote wanaonunua bidhaa za wizi kutoka kwa wahalifu hao ili kusaidia kutokomeza uhalifu wa panyarod wanaosumbua wananchi Jijini Dar es salaam.

" Kila siku tutoe taarifa ya mafanikio ya oparesheni hii ,pia panyaroad mnapowakamata wapigeni picha nakuwaweka mitandaoni ili wajulikane,hii oparesheni ninayoizindua leo isiwe ya kimyakimya ,Mambo matano niliyoyaelekeza yawe yakudumu kukabiliana na panyaroadi " amesem RC Makalla.
Naye Kamanda wa  Jeshi la polisi Kanda Maalumu Dar es salaam ACP Jumanne Muliro amesema mwezi Aprili Mwaka huu Jeshi hilo limeendesha opereshe nakufanikiwa  kuwakamata vijana wapatao 15 wenye umri kuanzia miaka 13  na kuendelea wanaosadikiwa ni  panyaroad nakwamba wanaendelea kushikiliwa kwamahojiano zaidi.

"Vijana wanaondelea na uhalifu mwisho wao umefika ,wazazi wao wawaonye watoto wao kwani kwa Sasa wakikamatwa watapigwa picha na kusambazwa katika mitandao ya kijamii ili wajulikane na ndugu zao wapate taarifa za haraka mahali walipo"amesisitiza Acp Muliro.

Vikundi vya Vijana maarufu Kama Panyaroad vimeanza kuibuka tena hivi karibuni huko Chanika Wilaya ya Temeke,Tabata wilayani Ilala  na Kunduchi wilaya ya Kinondoni na kuanza kufanya vitendo vya kiuharifu ikiwemo kuvamia na kukata mapanga nakujeruhi wananchi huku wakipora vitu mbalimbali.

No comments