Zinazobamba

Dkt Lwoga:Wasanii Tumieni Majukwaa Kutangaza Kazi Zenu za Sanaa ili Mtimize Ndoto Zenu.

Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga akizungumza wakati wa uzinduzi wa program ya Sanaa kwa Pamoja katika Makumbusho ya Taifa yaliyopo Posta Jijini Dar e s salaam mwishoni mwa wiki.

Na Mussa Augustine.

 Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt  Noeli Lwoga  amewashauri Wasiniii kupenda kutumia majukwaa au midahalo mbalimbali kuonyesha kazi zao ili kuwasaidia kujitangaza na kutimiza ndoto zao.

 Wito huo umetolewa mwashoni mwa wiki  Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa program ya "Sanaa kwa Pamoja" inayotekelezwa na Nafasi arts Space kwa kushirikiana na Makumbusho ya Taifa ili kwa lengo la  kuleta uwiano wa pamoja kwa vijana katika kazi  za Sanaa

 Dkt Lwoga amesema kwamba majukwaa yanayowakutanisha wasanii wa ndani na nje ya Nchi yanasaidia wasanii kutangaza vipaji vyao na kuviendeleza hivyo kuwafanya kujitengenezea ajira na kuondokana na utegemezi kwa walezi wao

 "Hakuna budi wasanii hawa wakatengenezewa majukwaa endelevu kwani walio wengi wanategemea kupitia majukwaa hayo ,wataonyesha kazi zao na zikionekana wanajipatia kipato kupitia watu watakaovutiwa na kuweza kuzinunua "amesema Dkt Lwoga

 Nakuongeza kuwa "taratibu taratibu kadri siku zinavyozidi kuendelea  wasanii wa Tanzania wanaendelea kuvuka mipaka kimataifa na kuipeperusha pendera ya nchi kupitia majukwaa na midahalo mbalimbali ,hivyo Serikali imekua bega kwa bega kuhakikisha vipaji chipukizi vinatengenezewa mazingira wezeshi. 




Naibu Mkuruge nzi Mkuu Tanzania bora Initiative ambayo ni sehemu ya Sanaa pamoja program kwa kushirikiana na Nafasi Arts Space Bw.Ismail Biro akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya uzinduzi wa program ya Sanaa kwa Pamoja
 Kwa upande wake Naibu Mkuruge nzi Mkuu Tanzania bora Initiative ambayo ni sehemu ya Sanaa pamoja program kwa kushirikiana na Nafasi Arts Space Bw.Ismail Biro amesema kuwa kupitia programu hiyo iliyozinduliwa itasaidia kuwasogeza wasanii pamoja kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali ikiwemo wanaoshiriki Sanaa Kwa vitendo,nadharia ili kusaidia kazi zao kuwa bora kimataifa. 

"Tutawatengenezea mazingira wasanii ya kuweza kupata fursa kupitia kazi zao wanazozifanya kwa kuwakutanisha na wadau mbalimbali wa Maendeleo ndani na nje ya nchi ili waweze kuwasaidia pale wanapokuwa na changamoto yoyote ili wafikie malengo wanayokusudia "amesema Bw.Ismaili

Kupitia Uzinduzi wa Programu ya "Sanaa Kwa pamoja"baadhi ya kazi za Sanaa ya uchoraji zimepokelewa na kuhifadhiwa kwenye Makumbusho ya Taifa ambapo miongoni mwa msanii aliyekabidhi kazi hizo ni Mwanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA) Mwamtumu Mburuku ambapo amewaasa  vijana  kujitokeza kuonyesha vipaji vyao.


Mwanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA) Mwamtumu Mbaruku akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) mara ya baada ya picha yake aliyotengeneza kupokelewa na kuhifaddhiwa kwenye makumbusho ya Taifa.

"Ninajisikia furaha sana picha yangu niliyoichora kupokelewa na kuhifadhiwa hapa makumbusho ya Taifa Mimi ni mwanafunzi mdogo na ni msanii mchanga nataumaini kupitia majukwaa ya Sanaa nitafika mbali na kutimiza ndoto yangu. amesisitiza Mwamtum

Naye Balozi wa Uswis Nchini Tanzania Didier Chassot amesema Ubolozi huo umetenga kiasi cha fedha  ambacho kitakuwa chachu ya  kuweza kuwasaidia wasanii ikiwemo wasanii wa nyimbo,Sanaa za maonyesho,Sanaa za uchoraji nazinginezo  hivyo  wasanii hao wachangamkie fursa hiyo.

Aidha Programu hiyo ya Sanaa Kwa Pamoja imefadhiliwa na wadau mbalimbali wa Maendeleo ikiwemo Umoja wa Ulaya(EU),Ubalozi Norwey ,pamoja na Ubalozi wa Uswis kiwa na lengo ni kusaidia kuzungumzia changamoto katika sekta ya sanaa na jinsi ya kuzitatua ili kuikuza sekta hiyo na kutengeza ajira kwa vijana.

No comments