Zinazobamba

Ujenzi wa shule ya Tamsya Dodoma kuanza mwakani, Rais Samia kuweka jiwe la msingi

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya wanafunzi na vijana wa kiislam Tanzania, (TAMSYA) Buliba Magambo amefichua kuwa Jumuiya hiyo inataraji kujenga shule katika eneo la Dodoma na wamepanga jiwe na msingi kuwekwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Rasi Samia Suluhu Hassan.




Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika hafla ya Ifatari Talks iliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha ualim DUCE, chang’ombe bosi huyo alisema tayari vitu vyote vilivyokuwa changamoto katika ujenzi vimepatiwa ufumbuzi.

“Habari njema kwa wanachama wa Tamsya ni kwamba katika ardhi yetu ya Dodoma ambayo inafikia ukubwa wa heka 7 tumeweza kumaliza mgogoro uliopo, pia tumeweza kulipa kiasi cha Shilingi million 14 ili kupata vibali halali vya umiki, hatua inafuata ni ujenzi wa shule,” alisema

Alisema ili kukamilisha jambo hilo kwa vitendo wamedahamiria kumkaribisha mama Samia kuweka jiwe la msingi.

“Tamsya ina utaratibu wa kufanya mkutano mkuu kila mwaka, mwaka huu tunaupeleka mkutano wetu mjini Dodoma, lengo ni kuwa karibu na eneo hilo la ujenzi,” alisema

                                                                                                        

Aidha akizungumzia hafla ya Iftari Talk iliyoandaliwa kwa ubia wa Tamsya na Ubalozi wa Uturuki, Magambo alisema hafla hizo zinasaidia kuwaunganisha wanavyuo na kupana fursa.

“Tamsya taifa tumeshirikiana na Rehma wakfu katika kuandaa iftarai Talks tukiwa na lengo la kuwaunganisha wanafunzi wa vyuo vya kati na vyuo vikuu vilivyopo Dar ess Slaam kwa lengo la kubadirishana nao mawazo,” alisema

Lengo kuu la tamsya ni kuwaunganisha vijana katika kupambana na ujinga, maradhi, umasikini na mmomonyoko wa maadili, tunawaeleza leo hapa ni vitu gani wanapaswa kuvifanya wakiwa chuoni na vitu gani waachane navyo,” alifafanua

Katika hafla hiyo ambayo imehudhuriwa na vijana Zaidi ya 500, vijana mbalimbali walionekana kufurahia hafla huku wakishauri uongozi kuendelea kuleta masheikh wakubwa kwa ajili ya kujifunza.

Aidh alisema wamejipanga kufanya kazi kwa karibu na viongozi wote wa ngazi ya Wilaya, Mikoa hasa katika kuhakikisha Jumuiya inafahamika vizuri katika ngazi ya shule ya msingi, tayari wameshafanya ziara mbalimbali kuangalia maendeleo ya Jumuiya.

 

Pia alitaja eneo lingine wanalowekeza nguvu ni kuwaunganisha wanafunzi wa vyuo vya kati na vyuo vikuu ambako kwa kiasi kikubwa kumeonekana kuna madhehebu mengi.

Wakizungumza katika hafla hiyo washiriki wa iftari hiyo, Iddi Hanzuruni Iddi mwanafunzi wa udaktari kutoka chuo cha St. Joseph ameelezea kuvutiwa kwake na hafla hizo akisisitiza kuwa zinawapa fursa ya kukutana (Networking).

Aidha amevutiwa na mada walizofundishwa ikiwamo njia nzuri ya kujali muda, kwani muda ndio kila kitu na ukichezewa hauwezi kurejea.

Pia ubunifu na ujio wa mada anuai zinachangia kuongeza vionjo vya hafla hizo na nawashauri vijana waweze kujitokeza kwa wingi kupata elimu inayotolewa katika hafla kama hizi.

TAMSYA ni jumuiya ya wanafunzi na vijana wa kislamu tanzania iliyoanzishwa mwaka 1993, ndiyo chombo pekee cha vijana wa kiislamu kilichofika mikoa yote na wilaya zake.

 

Miongoni mwa viongozi wakubwa ambao wamehudumu ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo na Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Bw. Kher James.

Heri James aliwahi kuhudumu kama Katibu mkuu wa mkoa wa Mwanza, hapo aliweza kupata uzoefu na umahili katika kujenga hoja pamoja na kuongoza mikutano mbalimbali.

Mpaka sasa wapo viongozi wengi ambao wapo serikalini na kwenye vyama na mashirika mbalimbali ya umma na binafsi ambao uzoefu wao wameupata kupitia tanuru la Tamsya.


Hakuna maoni