Zinazobamba

Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo awataka wana CCM kuelezea wananchi kazi zinazofanywa na Rais Samia.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo, amewataka Viongozi na wanachama wa chama hicho kuwa mstari wa mbele kuyasema mazuri yanayofanya na Awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo

Katibu Mkuu Chongolo ameyasema hayo katika ziara yake Wilaya ya Ilala ukumbi wa Arnatogluo, kuongea na Wajumbe wa Halmashauri Kuu wa Wilaya ya Ilala.

Aidha amewataka madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kufanya kazi ikiwemo kukagua Miradi ya maendeleo iliyopo katika kata zao sambamba na kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katibu Mkuu Chongolo amesema madiwani katika kata zao wafanye ziara na kukagua Miradi kutangaza utekelezaji wa Ilani unaofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inaongozwa na Rais wetu Samia Suluhu Hassan.

“Rais Samia amefanya mambo mengi kwa kipindi hiki cha mwaka mmoja katika sekta ya elimu kwa mara ya kwanza wanafunzi wote waliofaulu wameingia kidato cha kwanza baada ya ujenzi wa madarasa yakutosha Sekta ya Afya nayo amejenga vituo vya Afya vya kutosha hadi pembezoni mwa mji haya nayo sisi wana CCM tunatakiwa kuyasemea kwa wananchi “ Amesema Katibu Chongolo.

Hata hivyo ameipongeza Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ilala na Mkoa wanafanya kazi vizuri hususani katika kuratibu zoezi la upangaji wa utaratibu wa waendesha bajaji wenye Ulemavu na Bodaboda kuingia katikati ya Jiji pamoja na suala la usafi ambapo kwa sasa mji unavutia

“ Suala la Waendesha pikipiki Bodaboda na Bajaji CCM ipo karibu inafatilia kikubwa kuwawekea utaratibu sio kuwazuia kwani wengi wao Waendesha Bodaboda na Bajaji wamekopa mikopo ya serikali ya asilimia kumi ya Wanawake Vijana pamoja na watu wenye Ulemavu na inapaswa kurudishwa.

Sambamba na hayo amewataka Viongozi wa Chama hicho kwa ngazi mbalimbali kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa uadilifu na kuepuka masuala ya rushwa hasa kipindi hiki cha kuekekea uchaguzi huku akiwataka makatibu wa chama kufanya kazi zao bila kuegemea upande wowote wa wagombea nafasi za uchaguzi.

“Rushwa ni adui wa haki hivyo yeyote atakai kutwa na tuhuma za rushwa hiyo itakuwa juu yake binafsi na sio chama, tayari maafisa wa TAKUKURU wapo kwenye kazi yao, kiongozi mzuri hatoi rushwa wala kupanga safu ili achaguliwe bali utendaji wake wa kazi ndio utakao mpa nafasi ya kuwaongoza wenzake “Amesema Katibu Chongolo.

No comments