Zinazobamba

TGNP YAADHIMISHA MASAA 8760 YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN MADARAKANI.

Rais Samia Suhuhu Hassan amekuwa kiongozi wa kwanza wa nchi hii kujipambanua kuwa ukatili wa kijinsia ni kipaumbele chake, na kuahidi kuwa ataongeza idadi ya wanawake katika nafasi za uongozi na maamuzi kwa kuangalia vigezo.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akiongea na waandishi wa habari pamoja na wageni walio hudhuria katika kongamano la masaa 8760 ya Rais Samia Suluhu Hassan akiwa madarakani.

-ayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi katika Kongamano la masaa 8760 ya Rais Samia Suluhu Hassani tangu aingie madarakani.

Amesema kuwa Kongamano hilo limewakutanisha Wawakilishi kutoka Asasi za kiraia, Wanafunzi wa vyuo vikuu, Club za jinsia mshuleni Wanasemina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) na wanaharakati mbalimbali wa haki za wanawake na Watoto, huku lengo likiwa ni kupongeza kazi inayofanywa na serikali ya awamu ya sita.

Kongamano hilo lililofanyika makao makuu ya TGNP Mabibo mkoani Dar es salaam, Likiongozwa na kauli mbiu inayosema “Wanawake na Uongozi Kikazi Zaidi”

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa Kuna harakati kubwa sana zilifanyika huko nyuma hata kabla ya uhuru za kuhakikisha wanawake wanashika nafasi za uongozi mfano ukiwa ni wa Chief lity wa Singida, Chief Nduna Mkomalila wa Songea, Bibi Titi Mohamed, wakina Anna Makinda nk.

Ameendelea kusema kuwa wanawake waliyochaguliwa na Mh. Rais kushika nafasi hizo ambazo toka uhuru hazijawahi kushikwa na jinsi hiyo, Wanawake hao wameendelea kufanya vizuri Zaidi kuliko hata wanaume na hii inaleta picha kuwa wanawake wakipatiwa nafasi wanaweza.

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya TGNP, Gemma Akilimali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya TGNP, Dada Gemma Akilimali amesema kuwa licha ya mafanikio hayo yote lakini anatamani baadhi ya mambo yaweze kufanyiwa kazi ili nchi iendelee ku wa ustawi mzuri, ikiwemo vijana wanaomaliza elimu ya juu waweze kuangaliwa katika kupatiwa ajira na Si kuwalazimisha waweze kujiajiri wakati elimu ya kujitegeme hawakupatiwa tangu wakiwa mashuleni.

Ameongeza kuwa ni vema serikali ya awamu ya sita ikawekeza nguvu katika elimu ya kujitengemea ili mtoto anapomaliza elimu yake hata ya sekondari awe na uwezo kujiajiri mwenyewe na siyo mpaka subiri ajira serikalini.

Na mwisho ametoa maoni kuwa serikali ilitakiwa kuandaa mazingira wezeshi kwa wafanyabishara wadogo (wamachinga) kwa kuwaandalia maeneo ya kwenda kabla ya kuwatoa barabarani hali inayoleta sintofahamu kwani wafanyabishara wengi wanaoteseka ni wakina mama na vijana.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akiongea na waandishi wa habari pamoja na wageni walio hudhuria katika kongamano la masaa 8760 ya Rais Samia Suluhu Hassan akiwa madarakani.
Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali kulia akiandika point zinazoelezwa na wadau katika kongamano la masaa 8760 ya Rais Samia Madarakani.
Baadhi ya washiriki wa kongamano la masaa 8760 ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Masaa 8760 ya Rais Samia Suluhu Hassan Madarakani lililoandaliwa na TGNP.

No comments