Kamishna Kayera Awaasa Wanandoa Kumiliki hati ya Ardhi Kwa Pamoja ili kuepika migogoro
Na Mussa Augustine
Kamishna wa ardhi Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Idrisa Kayera amewaasa watu wanaoishi kwenye ndoa kuhakikisha wanapata hati ya ardhi kwa pamoja ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza endepo mmoja kati yao anaweza kufariki dunia.
Kamishina huyo ametoa rai hiyo mwishoni mwawiki ,katika viwanja vya mbagala zachiem wakati akikabidhi hati miliki ya ardhi kwa wakazi wa halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
Aidha amesema kwamba kumekuwa na migogoro mingi kwa baadhi ya familia itokanayo na hati miliki ya ardhi kutokana na wanandoa kushindwa kushirikishana kwa pamoja wakati wa mchakato wa kupata hati miliki ya ardhi nakwamba hati hiyo kuoneshajina moja la mwanandoa.
Amesisitiza kuwa hali hiyo inaleta sintofahamu kwenye masuala ya mirathi inapotokea mwanandoa mmoja kufariki dunia.
Rai hiyo ya Kamishna imekuja baada ya wanandoa wawili ambao ni Bw. Froldius Mutungi na mkewe Herieth Rugemalira kuhusika kufanya mchakato wa kupata hati kwa pamoja haliambayo inaleta mfano mzuri wa kuigwa kwa wanandoa wengine.
"Nivizuri kumilikishwa hati ya ardhi
mke na mume kwa pamoja ili kuepukana na migogoro inayojitokeza baada ya mmoja wa wanandoa anapotangulia mbele ya haki (kufariki)," amesisitiza kamishina Kayera.
Sanjari na hayo Kamishna Kayera amekabidhi hati miliki kwa wakazi 310 kutoka kata 14 za halmashauri ya wilaya ya Temeke,ambapo ametumia fursa hiyo kuwataka
wananchi waendelee kurasmisha maeneo yao ili wapate hati miliki ya ardhi itakayowasaidia katika masuala mbalimbali ikiwemo maendeleo yakiuchumi kutokana nakutumia kama dhama kwenyetaasisi za fedha ili kupata mikopo.
Wakati wa ugawaji wa hatimiliki za ardhi Kamishina Kayera amesisitiza jamiii kuiga mfano wa watu wanaoambatana na wake zao na kuweka majina yao kwemye hati zao kwani hali hiyo Ina ondoa migogoro wakati mmoja anapokuwa amefariki Dunia.
Naye mwenyekiti wa kibonde maji kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema zoezi hilo limefanyika kwa weledi mkubwa na kuwa limesaidia sana wananchi.
Katika zoezi hilo kata za Chamanzi,Toangoma,Makangarawe pamoja na Mbagala Kuu,Mianzini, harambe,Buza,Kijichi pamoja na kata zingine za Yombo vituka na Kibondeni.
Kwa upande wake afisa Mipango Wilaya ya Temeke Bi.Veronica Igoko aliyemwakolisha Mkurugenzi wa halmashauri hiyo amesema amewaomba wajumbe wanyumba 50 watoe ushirikiano wa kutosha katika zoezi la Anuani za Makazi .
Amsesema urasimishaji wa makazi unaendelea na ifikapo Agusti 2022 kutakuwa na zoezi la sensa ya watu na makazi na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa.
"Nawasihi sana wananchi waendelee kuchangia gharama za upimaji ilimuweza kupata hati miliki,hii itarahisisha wakandarasi kufanya wajibu wao Kwa urahisi na kuwawezesha wataalam wetu kurahisisha zoezi la ufuatiliaji na uwajibikaji na hatimaye hati ziendelee kutolewa."
No comments
Post a Comment