Zinazobamba

 Na Mussa Augustine.

Kampuni ya Movit Family Soap imezindua bidhaa zake mpya za sabuni ambazo zimetengenezwa kwa ladha nne tofauti ili kuendelea kuwapatia watanzania bidhaa bora wanazohitaji.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Bidhaa hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo hapa Nchini  Oscar Ntorinwe amesema kwsamba wameamua kuzindua bidhaa hizo kutokana na kufanya utafiti kwenye Kipindi cha mripiko wa ugonjwa hatari wa Corona nakubaini kwamba watanzania wanahitaji bidhaa bora ya sabuni kwa ajili ya kufanyia usafi.

Amesema kwamba bidhaa hiyo kwa sasa inapatikana kwa mawakala nchini kote nakwamba huku akisistiza kwamba kampuni hiyo ya Movit itaendelea kuwaletea Watanzania  bidhaa zenye bora unaotakiwa.

“Leo tunazindua sabuni za “New Movit Family Soap” ambazo zimetengenezwa na kampuni yetu ya Movit ,tumezingatiwa viwango vya ubora na tunapenda kuwambia watanzania wazitumie sabuni hizi kwani zinatumika kwa rika lote ikiwemo watoto na watu wazimi,pia zinapatikana kwenye maduka mbalimbali ya vipodozi pamoja na mawakala wetu”amesema Meneja huyo.

Kwa upande wake Elizabert Lema ambaye ni mwanafamilia wa Kampuni ya Movit Family Soap kwamba sabuni hizo mpya zimetengenezwa kwa ladha tofauti ikiweo Lemon,Coconut,Rose pamoja Alovera nakwamba zinakidhi mahitaji ya watanzania.

Tuna bidhaa za aina nne ambazo tunazindua leo ,tuna sabuni iliyotengenezwa kwa Lemon,Rose,Coconut na Alovera na tunaamini watanzania wanapata sabuni nzuri zinazoendana na ngozi zao kwani tumefanya utafiti ndo tukaja na bidhaa hizi ambazo ni suluhisho la usafi wa ngozi hivyo watanzania wazitumie”amesema Elizabert.

Nae Mosco Stevin ambaye ni wakala wa Sabuni za Movit Family Soap Kariakoo jijini Dar es salaam amesema kwamba sabuni hizo zinauwezo mkubwa wakulinda ngozi nakwamba zimekuwa bora zaidi katika ushindani wa soko uliopo kwa sasa.

Hakuna maoni