Mufti Tanzania ataka Waislam kuacha kulalamika
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari Zubeir amewataka vijana wa kiislam kuacha kulalamika kuhusu furasa za ajira na badala yake wajikite katika matayarisho ili wawe na sifa ya kuzipata zitakapotokea.
Mufti
amebainisha hayo katika mashindano ya quran yanayoandaliwa na Taasisi ya
Istiqaama yenye Makao Makuu yake jijini Dar es Salaam.
Alisema
watanzania wengi wamekuwa na tatizo la kulalamika jambo ambalo amelikemea na
kuweka wazi kuwa halina afya kwa mustakabali wa vijana.
Kwa
upande wake, Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),
Mhe. Dkt. Selamani Jafo amewaasa wazazi na wadau mbalimbali kuhakikisha vijana
walioweza kuhifadhi kitabu cha mwenyezi Mungu wayaishi maisha yanayo akisi
kitabu Allah.
Alisema
Wazazi wana kazi kubwa ya kufanya, wameweza kuwasimamia katika hatua za awali
hadi kufikia mafanikio ya kuhifdhi kitabu kitukufu, basi waendelee na kazi hiyo
ili kuwafanya watoto hao wasibadilike mienendo.
Alisema
wazazi wakifanikiwa hapo watakuwa wamefaulu kwani wataacha mtoto mwema ambaye
atakuja kumuombea dua mara tu watakapo ondoka katika mgongo wa ardhi.
Akizungumza
katika hadhara ya mashindano ya quran yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama
Muslim Community Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa NSSF uliopo Ilala Jijini
Dar es Salaam, Jafo alisema malezi kwa vijana hawa yanapaswa kuendelea.
Vilevile
Waziri Jafo amewapongeza Taasisi ya Istiqaama kwa kuendelea kuandaa mashindano
hayo, akisema yamekuwa na tija kwa maendeleo ya taifa la Tanzania
“Vijana
walioweza kuhifadhi kitabu cha mwenyezi Mungu wanaweza mambo mengi, vijana hawa
wakipewa dhamana watakuwa na hofu ya mwenyezi Mungu,” alisema
Pia
alieleza kufurahishwa kwake kwa kitendo cha mashindano hayo kuhusisha na upande
wa pili wa muungano, kwani anaamini hilo ni jambo zuri lenye kustawisha
muungano.
Aidha
Jafo hakusita kuonyesha furaha yake kwa kukithiri kwa mashindano ya quran
katika miaka ya hivi karibuni na kusema mashindano hayo yanachangia kustawisha
Amani.
“Nimefurahi
kuona mwendelezo wa mashindano ya quran, April 9, yamefanyika haya ya
Istiqaama, April 10, yapo ya Bi Aisha Sururu, April 16, yapo yale ya Asb hab
QAF pale viwanja vya sabasaba, April 17, yapo yale ya bara la Afrika
yatakayofanyika uwanja wa taifa na kuandaliwa na Al-hkma Foundation, April 24
tunamaliza na mashindano makubwa ya dunia yanayoandaliwa na jumuya ya
kuhifadhisha quran chini ya Sheikh Kaporo, matukio yamepanga yakapangika ni rah
asana kwa wapenzi wa quran,” alisema.
Pia
Jafo amewatia moyo wanachama wa Taasisi ya Istiqaama Muslim Community Tanzania
kwa michango yao wanayotoa kuboresha chama kwani kazi wanayofanya ni uwekezaji
mkubwa kwa mwenyezi Mungu.
“Kinachofanyika
katika kusomesha vijana kusoma quran na kuhifadhi huu ni uwekezaji wa hali ya
juu sana, inawezekana watu wasifahamu hilo, lakini ni wazi kuwa tunawekeza
mbele za Allah,” alisema
Akizungumzaia
juu ya serikali kuunga mkono juhudi zinazofanyawa na Taasisi zinazoandaa
mashindano ya quran, Waziri Jafo alisema Serrikali ya awamu ya sita
inayoongozwa na mama Samia Suluhu Hassani inaunga mkono Taasisi zote za dini,
kwani inajua wazi kuwa Amani haiwezi kupatikana bila kuwa na vijana wenye
maadili mema.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Seif Ali alipongeza wanachama wa
Taasisi ya Istiqaama Muslim Community Tanzania kwa michango yao wanayoitoa na
kuwaomba kuendelea kutoa kwani uhai wa chama ni michago
“Mwaka
jana tulizindua mfumo wa kuchangia chama, kwa sababu ya corona mambo hayakwenda
vizuri, lakini wapo waliochangia, mpaka tunafunga mwaka tumepata Mil. 35,
tunaamini michango hii itaongezeka tukizingatia kuwa sasa hali imetulia,”
alisema
Aidha
alisema, Taasisi ya Istiqaama Muslim Community Tanzania inafikilia kujenga
Mahadi huko Kigamboni, Jijini Dar es salaam, wanawaomba wanachama kuongeza kasi
ya michango.
“Jumuiya
yetu inamatawi 25 hapa nchini, tukiangalia hamasa ya usomaji qurani kwa kweli
imeongezeka, nguvu inayotumika imeanza kuleta matunda kwa vijana wengi kupenda
kusoma qurani,” alisema
Kwa
upande wake mshindi wa jumla wa mashindano hayo amewaomba vijana kufanya juhudi
ya kukisoma kitabu cha Allah akisisitiza kuwa hakuna kinachoshindikana kama
umefanya maamuzi.
Alisema
ushindi wake umetokana na juhudi alizokuwa akifanya kwa kushirikiana na Sheikh
wake, huku akisema hakuamini kama siku moja angeweza kuibuka kuwa mshindi wa
juzuu 30.
Naye
mratibu wa mashindano hayo Bw. Khalifa Seif alisema mashindano yam waka huu
yamepata mafanikio makubwa kwani vijana wengi walijitokeza kushiriki.
Aidha
Khalifa ameungana na Mgeni Rasmi kwa kutoa wa vijana waliohifadhi quran
kuendelezwa na elimu zote mbili, ikiwamo ya sekula na dini.
“Watoto
wetu wamejitahidi sana katika mashindano haya, wito wangu watoto hawa
waendelezwe ili kuweza kupata watoto bora Zaidi, yeyote aliyebeba quran atakuwa
bora katika kazi zake lakini hata katika taifa lake,” alisema
“Mimi
ndio Kiongozi Mkuu wa kamati ya daawa, kamati ya quraan, ujenzi wa Mahad ni
jambo muhimu sana kwa mustakabali wa Jumuiya na waislam kwa ujumla
Hiyo
ni kwa sababu kila kitu kinahitaji elimu, na mahadi ni nyumba ya elimu,
ishaalah Mahd hii iko njiani kujengwa ni mahadi kubwa ambayo itachukua
wanafunzi kuanzia kazi ya msingi ya iptidaiya, thanawi mpaka jamiya,”
alisisitiza.
Amewaomba
waislam kushiriki katika kheri hizi ili kufanikisha ujenzi wa Mahdi hiyo ambayo
ni habari njema kwa waislam. Eneo inapotarajiwa kujengwa kwa Mahdi hiyo ni
Mwasonge karibu na Dar es Salaam Zoo, kuna kiwanja cha Istiqaama kisichopungua
heka 50, chuo kitajengwa hapo.
No comments
Post a Comment