Zinazobamba

Serikali imeombwa kuendelea na mchakatio wa kufanyia marekebisho sera ya Taifa ya Uwekezaji.

Na Mussa Augustine.

Serikali kupitia Wizara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara imeombwa kuendelea na mchakato wa  kufanyia marekebisho sera ya Taifa ya Uwekezaji ili kuendana na kasi ya Uwekezaji unaoendelea hapa nchini

Mkurugenzi Mkazi wa Trademark East Africa (TMEA) Monica Hangi.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkazi wa Trademark East Africa (TMEA) Monica Hangi wakati wa Mkutano wa Wadau wa Uwekezaji uliyofanyika jijini Dar es salaam ikiwa lengo ni kujadili sera mpya ya uwekezaji mwaka 2022.

Mkurugenzi huyo amewaambia waandishi wa habari kando ya Mkutano huo kuwa Sera ya Uwekezaji iliyopo kwa sasa inahitaji kuongezewa baadhi ya mambo ikiwemo masuala ya rasilimali pamoja na upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kuwekeza kwenye sekta mbalimbali.

Baadhi ya washiriki wakifuatilia mkutano.

“Tumefanya kazi kwa muda mrefu kwa kushirikiana na Wizara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara ili kufanyia marekebisho sera ya Uwekezaji,tumejadili kwa kina na tunaendelea na majadiliano,tunaiomba serikali iharakishe suala hili ili kusaidia kuendana na kasi ya wawekezaji ambao wanakuja kwa wingi kuwekeza hapa nchini”amesema Monica.

Nakuongeza kwamba “Serikali ya awamu ya Sita inayongozwa na Rais Samia Suluhu Hassani imefanikiwa kwa Kiasi kikubwa kufungua milango ya uwekezaji hivyo hakuna budi kuwa na sera nzuri ya uwekezaji itakayowafanya wawekezaji waendeleee kuja kuwekeza hapa nchini.

Afisa Biashara na Uchumi kutoka Ubalozi wa Uholanzi hapa nchini Caroline  Kibinga.

Kwa upande wake Afisa Biashara na Uchumi kutoka Ubalozi wa Uholanzi hapa nchini Caroline  Kibinga amesema sera ya uwekezaji iliyopo kwa sasa imekuwa na changamoto mbalimbali hivyo kupitia mkutano huo wa wadau itasadia kujadili kwa pamoja na kutoa mapendekezo yao kwenye maeneo yanayopaswa kufanyiwa marekebisho.

“Tanzania imefunguka katika masuala ya Biashara na Uwekezaji hivyo tunataka kufanyiwa marekebisho katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuwepo kwa majumuisho ya pomoja ya mifumo ya uwekezaji kuanzia masuala ya Usajili hadi taratibu nzima za uwekezaji kukamilika”amesema Caroline

Tim Green kutoka Ubalozi wa Uingereza hapa nchini.

Pia Tim Green kutoka Ubalozi wa Uingereza hapa nchini amesema kwamba Tanzania ni nchi nzuri kwenye masuala ya uwekezaji kwani sera zake za Uwekezaji zimekuwa zikiwavutia wafanyabiashara wengi hapa nchini na kwamba sera hizo zinatakiwa kufanyiwa marekebisho ili ziwe bora zaidi.

Mkutano ukiendelea.

Hakuna maoni