Wawekezaji kutoka Qatar wakiwa katika mkutano wa majadiliano katika ofisi za Tic jijini Dar es salaam.
Na Mussa Augustine.
Kituo Cha Uwekezaji Nchini
(TIC) kimepokea wawekezaji wapatao 25 kutoka Nchini Qatar ambao wamekuja
kuangalia fursa za Uwekezaji katika sekta mbalimbali hapa Nchini.
Akizungumza na wanahabari
Mara baada ya kupokea wawekezaji hao Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Bi. Anna
Lyimo amesema ujio wa wawekezaji hao unatokana na ziara iliyofanywa hivi
karibuni na Viongozi wa TIC ambao walienda nchini Qatar nakufanya
mazungumzo na baadhi ya Wafanyabiashara kutoka shirikisho la Wafanyabiashara la
Qatar KERALA BUSINESS FORUM.
" Ujio wa wageni hawa
unatokana na mwendelezo wa kuhamasish na kuwavutia wawekezaji,hivyo wawekezaji
wapatao 25 wamekuja kuangalia fursa ya kuwekeza Kati sekta mbalimbali ikiwemo
Mifugo,Vifaa tiba,Utalii,Madawa, sekta ya anga pamoja na masuala ya uchumi wa
Bluu" amesema Anna.
Aidha amesema Kwamba kutokana
na kuwepo kwa diplomasia nzuri ya Uwekezaji pamoja na kufungua milango kwa
wawekezaji hao wawekezaji wengi wa kigeni wameanza kujitokeza huku akiwasihi
wawekezaji wa ndani wajiunge na TIC waweze kupata taarifa mbalimbali za fursa
ya Uwekezaji Nchini.
Amendelea kusema kuwa
wawekezaji hao wanatarajiwa Machi 29 kutembelea Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
kuangalia fursa ya Uwekezaji lakini kwa Sasa TIC inawapitisha katika taratibu
mbalimbali za Uwekezaji pamoja na masuala ya vibali vya kuwekeza Nchini.
Kwa upande wake Raisi wa
Shirikisho la wafanyabiashara Nchini Qatar Bw.Shanavas Bava amesema kwamba
wamekuja kuangalia fursa zakuwekeza hapa Nchini kutokana na Tanzania kuwa na
fursa nyingi lakini pia kuwepo na mazingira mazuri yakiuwekezaji ni jambo lililowavutia
kuja kuwekeza.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa
Lanchi ya Taifa( NARCO) Bw. Petter Msofe amesema mazao mengi ya Mifugo Kama
vile nyama ya Mbuzi,Ng'ombe na Kondoo yamekuwa yakitumika sana Mjini Doha
Nchini Qatar hivyo wawekezaji hao watasaidia kikuza sekta ya Mifugo
nakuongeza pato la Taifa.
" Hivi karibuni
tulihudhulia mkutano mkubwa wa Kilimo na Mazingira uliyofanyika mjini Doha
Nchini Qatar,tulishirikiana na ofisi ya balozi wa Tanzania Nchini Qatar,Doha
wanapenda sana kula nyama inayotoka kwetu hivyo wawekezaji wameanza kuja
kuwekeza, na sisi tunaendelea kuunga Mkono serikali ya rais Samia Suluhu Hassan
ambaye ameonyesha nia ya kufungua milango ya uwekezaji"amesema Be.Msofe.
No comments
Post a Comment