Kampuni ya Sukari Kilombero yawasihi Wafanyabiashara Kuacha Kupandisha Bei Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Na Mussa Augustine.
Kampuni ya Sukari Kilombero imewasihi Wafanyabiashara wote
wa jumla na rejareja wanaouza bidhaa za "Bwana Sukari kutokupandisha bei
kuelekea mfungo wa ramadhani unaotarajiwa kuanza mwanzo mwa mwezi aprili mwaka
huu ili kusaidia kuepuka taharuki inayoweza kujitokeza kwenye kipindi Cha
mfungo wa Mwezi Mtukufu wa ramadhani.
Tamko hilo limetolewa Jijini Dar es salaam na Mkuu wa idara
ya biashara wa kampuni ya Sukari kilombero Bw.Fimbo Butallah wakati akizungumza
na wanahabari kutokana na historia yakupanda kwa bei ya bidhaa za vyakula kila
uanzapo mfungo wa mwezi Mtukufu wa ramadhani nakusababisha adha kubwa kwa
waumini wanaofunga mwezi huo.
Aidha Butallah amesema katika uchumi wa soko huria wao Kama
wazalishaji hawaruhusiwi kuwapangia Wafanyabiashara bei yakuuza bidhaa lakini
wanawajibu mkubwa wakuwashauri upandishaji holela wa bei hasa pale ambapo
wazalishaji hawajapandisha bei ya bidhaa hiyo.
" Tunawasihi Wafanyabiashara kote Nchini kutopandisha
bei ya Sukari katika Mwezi Mtukufu wa ramadhani ili kuepuka taharuki inayoweza
kujitokeza " amesema kuu huyo wa idara ya biashara wa kampuni ya Sukari
Kilombero.
" Tumekwisha anza taratibu za uagizaji wa Sukari ambayo
inatarajiwa kuanza kuingia nchini muda wowote kuanzaia hivi Sasa tunapenda
kuwatoa hofu wananchi kuhusu upandaji holela wa bei ya Sukari hususani chapa ya
" Bwana Sukari" kwani kampuni imeandaa mikakati thabiti kukabiliana
na tatizo hilo katika msimu huu" amesema Butallah.
Kampuni ya Sukari ya Kilombero ambayo inamilikiwa na Kampuni
ya An illovo Sugar Africa kwa asilimia 75 na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa asilimia 25, ipo katika maandalizi ya Mradi wake wa upanuzi ambao
utakuza uwezo wa kampuni hiyo wa kuzalisha Sukari na kupunguza uhaba wa Sukari
Nchini kupitia chapa yake ya "Bwana Sukari"

No comments
Post a Comment