SERIKALI YAOMBWA KUWEKEZA KWENYE KIWANDA CHA KUZALISHA VIUADUDU VYA KUUA VILUILUI VYA MAZALIA YA MBU WA MALARIA
Mwenyekiti wa kamati ya Bajeti ya Bunge Daniel Sillo mwenye suti akizungumza na waandishi wa habari kwenye kiwanda cha kutengeneza dawa ya kuua viluilui vya mazalia ya mbu kilichopo katika kongani ya Viwanda ya NDC iliyopo kibaha Mkoani Pwani.
Na Mussa Augustine
Kamati ya Bajeti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema itaishauri serikali iweze kuwekeza fedha za kutosha kwenye kiwanda Cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluilui vya mazalia ya Mbu wa Malari ili kukifanya kiwanda hicho kifanye kazi kwa ufanisi mkubwa nakuweza kutokomeza ugonjwa na Malaria Nchini.
Hayo yamebainishwa leo na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Daniel Sillo wakati kamati hiyo ilipotembelea kiwanda hicho ambacho kipo chini ya Shirika la Maendeleo Nchini ( NDC) kilichopo kongani ya viwanda ya Shirika hilo iliopo Kibaha Mkoani Pwani.
Bwana Sillo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Mkoani Manyara amesema Kwamba kiwanda hicho kimekumbwa na changamoto mbalimbali hivyo ni wakati Sasa serikali kuwekeza katika kiwanda hicho ambacho kinasaidia katika kuzalisha dawa za kuua viluilui vya Mbu wa Malaria nakwamba dawa hizo zitauzwa ndani na nje ya nchi nakusaidia kulingizia Taifa kipato.
Amesema Kwamba kwasasa kunachangamoto yakupata ithibati kutoka shirika la Afya Duniani( WHO) ili kuzifanya dawa zinazozalishwa kwenye kiwanda hicho ziweze kuuzwa katika mataifa mengine,nakwamba mchakato wa kupata ithibati hiyo tayari umeshaanza kufanyika.
"Sisi Kama kamati ya Bajeti tutaishauri serikali iweze kutenga fedha kwenye Bajeti ya mwaka 2022/ 2023 zakuweza kukisaidia kiwanda hiki,na kwasasa kinazalisha bidhaa ambazo zinakiwango kinachotakiwa ,kilichobaki ni kupata ithibati kutoka WHO ili tuuze kwenye Nchi zingine za kimataifa ambapo tutalingizia taifa fedha nyingi sana kutokana na dawa hizi" amesema Sillo.\
\
Naibu Waziri wa Uwekezaji ,Viwanda na Biashara Axaud Kigahe mwenye miwani akizungumza na wanahabari kufafanua jambo katika kongani ya viwanda ya NDC iliyopo kibaha Mkoani Pwani mara baada ya Kamati ya Bajet ya Bunge ilipotembelea kiwanda cha kutengeneza dawa ya kuua viluilui vya mazalia ya Mbu.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Axaud Kigahe ameiambia kamati hiyo kuwa tayari serikali imeanza kuchukua hatua za kukinusuru kiwanda hicho ambacho kilikua kinakumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kushindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi,pamoja na huduma zingine zakiuendeshaji.
Amesema Kwamba serikali imetenga zaidi ya kiasi Cha shilingi bilioni 60 kwa ajili ya kulipa mishahara ya wafanyakazi lakini pia kuna madeni ya mifuko ya jamii yaani NSSF ambayo wafanyakazi walikua hawajalipiwa, kwasasa tayari wamelipiwa,changamoto zingine tunaendelea kuzifanyia kazi ili kiwanda hiki kiweze kuzalisha dawa za kutosha na zinazokidhi vigezo vya shirika la Afya Duniani"amesisitiza Naibu Waziri Kigahe.
Mkurugenzi mtendaji wa NDC Dr.Nicholaus Shombe akizungumza na wanahabari kweneye kiwanda cha kuzalisha Viua Dudu Vya Kuua Viluilui Vya Mbu wa Malaria Kihaba Mkoa wa Pwani.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Dr.Nicholaus Shombe amesema Kwamba kwa Sasa kiwanda hicho kinazalisha dawa kwa asilimia 20 ,hata hivyo dawa hizo za kuulia viluilui vya mbu zimeanza kuuzwa katika Nchi za Angola,Kenya , Swaziland, Uganda ,Niger, nakwamba uzalishaji mkubwa unahitajika ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje.
Amesema kwamba kiwanda hicho kinauwezo wakuzalisha bidhaa zingine Kama vile Mbolea isiyokua na kemikali,Dawa yakunyunyuzia mimea,pamoja na nyongeza za lishe hivyo shirika hilo linaendelea kushirikiana na serikali pamoja na sekta binafsi katika kutafuta masoko ya bidhaa hizo ndani na nje ya Nchi.
" Hiki ni kiwanda kikubwa sana ambacho kipo chini ya NDC ,kiwanda hiki kinazalisha dawa za kuua viluilui vya Mbu kwa kiwango Cha asilimia ishirini,lakini mahitaji yanayohitajika kwa Nchi yetu kwa mwaka ni tani milioni tano,hivyo tunahitajika kuendelea kuwekeza kwa nguvu zote ili kiwanda hiki kifanye kazi kwa ufanisi mkubwa nakuzalisha bidhaa zinazojitosheleza kulingana na mahitaji" amesema Dr. Shombe
Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi wapende kutumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani kwani kupitia dawa hiyo ya kuua viluilui vya mazalia ya Mbu shirika la Afya Duniani(WHO) limeikubali dawa hiyo nakwamba Tanzania ipo kwenye mazungumzo na WHO ili kupatiwa ithibati ya kuuza dawa hizo katika Nchi za Africa na Dunia kwa ujumla.
No comments
Post a Comment