Zinazobamba

NDC YAWATAKA WANAWAKE WACHANGAMKIE FURSA YA UWEKEZAJI WA VIWANDA

 

 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Dr.Nicholaus Shombe pichani hapo juu akizungumza na waandishi wa habari katika banda la shirika hilo kwenye maonyesho ya siku ya Wanawake Duniani yanayofanyika viwanja vya Mnazi Mnoja Jijijini Dar es salaam

Na Mussa Augustine

Ikiwa leo ni kelele cha Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani serikali kupitia Shirika la Maendeleo Nchini (NDC) imesema itahakikisha inaboresha mazingira ya uwekezaji wa Viwanda ili kuwafanya wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wavutiwe  kuwekeza miradi mbalimbali itakayo chochea ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa Ujumla.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa Shirika ilo Nicholaus Shombe wakati akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaamu wakati akielezea mikakati iliyojiwekea  NDC katika kuhakikisha inawanufaisha wawekezaji katika masuala ya Uwekezaji wa Viwanda.

Dr.Shombe amewaomba Watanzania waendelee kuliamini Shirika lao la Maendeleo la Taifa(NDC) kwasababu lina miradi mikubwa ambayo inatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa ya viwanda nakwamba tayari kuna baadhi ya wawekezaji kutoka mataifa yakigeni yameonyesha nia yakuwekeza katika viwanda vya kuunganisha magari.

Mkurugenzi huyo Mtendaji amesema Kwamba NDC kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Nchini ( TANESCO) wameanza kutatua kero ya kukatika kwa umeme Mara kwa Mara,pamoja nakuimarisha mfumo wa upatikanaji wa maji ya uhakika ili kuwafanya wawekezaji wawe na mazingira bora ya Uwekezaji.

Afisa Uhusiano wa NDC Mirian Chavalla wa kwanza kushoto akitoa maelezo ya miradi mbalimbali inayotekeleza na shirika hilo mbele ya Mkurugenzi Mtendaji Dr. Nicholaus Shombe wakati alipotembelea banda la shirika hilo Katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jiji Dar es salaam

"Tuna miradi mingi mikubwa ambayo tunaitekeleza,kuna Mradi wa Magadi Soda Mradi huu nimkubwa sana,ukizungumzia Makemoko ya Viwanda unazungumzia Magadi soda ,hivyo nawaomba Watanzania waendelee kuliamini Shirika lao la Maendeleo, namimi nikiwa kama mkurugenzi mtendaji kwa kushirikiana na timu yangu tutahakikisha tunaleta mabadiliko makumbwa ndani ya shirika " amesema Dr.Shombe.

 Nakuongeza kwamba "Tunataka tuwe na NDC yatofauti, shirika lipo kwa ajili yakuwasaidia watanzania,na maadhimisho haya ya siku ya mwanamke Duniani tupo hapa kuwambia wanawake kwamba NDC ipo kwa ajili yao ,wachangamkie firsa ya uwekezaji wa viwanda.

Aidha amewataka wanawake kuelekea maadhimisho yasiku ya mwanamke Dunia inayoazimishwa Machi 8 kila mwaka ,wajitokeze kuchangamkia fursa ya uwekezaji wa viwanda vya nguo kwenye kongani ya Viwanda ya NDC iliyopo kibaha Mkoani Pwani ili kuwafanya wanawake wazawa wanufaike na Viwanda.

Dr.Shombe ambaye ametembelea maonyesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wanawake kupitia viwanda vidogo ambayo yanafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam,ambapo amefurahishwa na kazi kubwa wanayoifanya.

 

 

No comments