PAUL KIMITI :AZUNGUMZIA MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 100 YA BABA WA TAIFA JULIUS KAMBARAGE NYERERE
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Paul Kimiti (pichani juu) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya maadhimisho ya miaka mia moja ya kuzaliwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yanayotarajiwa kufanyika april 13 mwaka huu.
Na Mussa Augustine
Taasisi
ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere inatarajia kufanya makongamano
yakumuenzi baba wa Taifa hayati Julius Kambarage Nyerere ikiwa ni sehemu ya
kuadhimisha kumbumkumbu ya Miaka 100
tangu Kuzaliwa kwake mwaka 1922.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es
salaam Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mheshimiwa Paul Kimiti amesema kwamba ifikapo
Aprili 13 baba wa Taifa atakua anatimiza miaka100 tangu Kuzaliwa, hivyo
makongamano hayo yatafanyika kikanda yakienda sambamba nakufanya shughuli za
kumuenzi baba wa Taifa katika mikoa yenye historia zake,pamoja na kuendeleza
agenda yakitaifa ya Upandaji wa miti.
Aidha
Kimiti amesema kwamba Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi za
uhai wake alisimamia falsafa ya kulinda amani ,kuondoa ubaguzi, nakuwafanya
Watanzania waweze kuishi kwa upendo,mshikamano pamoja na kujitegemea,ambapo falsafa hizo zinapaswa
kuenziwa kupitia Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu nyere ili
kuwafanya vijana na jamii kwa ujumla kuzifahamu.
Aidha
Mwekiti huyo ameongeza kwamba jamii inapaswa kuendelea kuzijua kazi
alizozifanya baba wa Taifa katika kulikomboa Taifa nakwamba kuenzi juhudi hizo
kutalifanya Taifa kuendelea kulinda misingi ya amani,mshikamano na upendo
nakuondoa ubaguzi miongoni mwa jamii ya kitanzania.
"
Mwalimu Nyerere angekua hai April 13 angetimiza
Miaka mia moja tangu Kuzaliwa kwake,tumeamua kufanya kumbukumbu ya
Kuzaliwa kwake kwa kufanya makongamano ambayo yatafanyika kikanda natutafanya
shughuli Mbalimbali za kumuenzi kikanda,tutanzia kanda ya Ziwa pale Butiama alipozaliwa,kanda
ya kaskazini,kanda ya kati (Dodoma) ,Kanda ya kusini na Kanda ya Magharibi,na
kumalizia Dar es salaam na Zanzibar” amesema Kimiti.
Nakusisitiza
kwamba" kila Kanda kutafanyika shughuli katika mikoa yenye historia
za Mwalimu Nyerere na Taifa kwa ujumla, pamoja na kufanya zoezi la Upandaji
miti, kutakua na makongamano yatakayozungumzia falsafa za mwalimu kulingana na
historia ya mikoa iliyopo kwenye Kanda hizi jinsi ilivyohusika katika
kuendeleza kudumisha amani,upendo na mshikamano.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Simon
Lubugu amesema kwamba viongozi waliopo kwa Sasa ni wale waliozaliwa Miaka
ya hivi karibuni hivyo hawajui misingi ya baba wa Taifa ilivyokua ,hivyo
kupitia Taasisi hiyo watapata fulsa yakujua misingi ya baba wa Taifa
aliyowajengea Watanzania enzi ya uhai wake.
"
Viongozi wengi wa Sasa wamezaliwa Miaka ya themanini hivyo wamekua sio
wazalendo kwa Taifa kwansababu hawajui misingi iliyoachwa na muasisi wa Taifa
hili,kuanzishwa kwa Taasisi hii itasaidia Sana vijana hawa waliozaliwa kipindi
hiki na kijacho kufahamu misingi hiyo iliyoachwa na Baba wa Taifa."
Amesema Lubugu.
Mjumbe wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu DOKII wakwanza kutoka mkono wa kulia akiwa na Mhamasishaji wa Taasisi hiyo Mtiti Mbassa Jirabi aliyepo katikati wakisikiliza ujambo kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Paul Kimiti hayupo pichani wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam
Mjumbe
wa Taasisi hiyo Ummy Wenceslaus alimaarufu kwa jina la “DOKII” amewasisitiza
vijana kuona umuhimu wakujiunga na Taasisi hiyo kutokana na mchango wa baba wa katika
kulijenga Taifa la Tanzania pamoja na mataifa mengine hasa katika kujenga
misingi ya amani,mshikamano na upendo pamoja na kuzisaidia baadhi ya nchi za barani
afrika kupata uhuru.
Halikadharika
amewataka wasanii kutumia sanaa zao kupaza sauti juu yakumuaenzi baba wa Taifa
katika jamii ili kuendeleza mazuri ambayo ameacha kama alama ya upendo
kwa Taifa,huku akiwaasa pia viongozi walioko madarakani kuyaishi kwa vitendo
yale yote aliyoanzisha baba wa Taifa.
"Ni
vyema viongozi wa sasa waziishi falsafa za baba wa Taifa kwa vitendo kwani
falsafa zake zimesaidia kuleta ukombozi
kwa Taifa na mataifa mengine Barani Afrika."Amesisitiza Dokii.
Mkutano
huo na waandishi wa habari umefanyika katika ofisi za taasisi hiyo zilizopo
Makonde Beach Dar es salaam na umeudhuliwa pia na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi
wa Taasisi hiyo Balozi Mstaafu Francis Mndolwa, pamoja na mhamasishaji wa
taasisi hiyo Mtiti Mbassa Jirabi ambao kwa nyakati tofauti wameelezea umuhimu
wa kumuenzi baba wa Taifa hayati Julius Kambarage Nyerere.
No comments
Post a Comment