MKINGA: WANAOEGESHA MAGARI WALIPE USHURU KWA WAKATI WAEPUKE USUMBUFU
Meneja wa Tarura Mkoa wa Dar es salaam Geofrey Mkinga akizungumza na mwandishi wa mtandao huu (hayupo pichani) wakati wa mahojiano maalumu ofisini kwake.
Na Mussa Augustine
Mamlaka ya Usimamizi wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Dar es salaam imewataka wamiliki wa magari kujisajili kwenye mfumo mpya wa kieletroniki ulioanzishwa na rasmi na mamlaka hiyo kwa ajili ya kuwasaidia kulipa ushuru wa maegesho kwa kutumia njia ya mdandao wa simu za mkononi.
Mamlaka hiyo pia imewataka wamiliki wa magari wanaoingia maeneo ya katikati ya jiji la Dar es salaam walipe ushuru wa maegesho kwa wakati ili kuepkana na usumbufu unaoweza kujitokeza .
Rai hiyo imetolewa na Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es salaam Geofrey Mkinga wakati akifanya mahojiano maalumu na Mtandao huu ofisisni kwake ambapo amebainisha kwamba mfumo wa kielektroniki wa ”TeRMIS APP” ulioanzishwa na Mamlaka hiyo umelenga kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali lakini pia unamsaidia mteja kuondokana na usumbufu unaojitokeza wa kulipa ushuru wa maegesho kwa kupitia risiti za kawaida.
Aidha Meneja
Mkinga amesema kwamba wateja ambao wanafanyabiashara zao kwa muda mrefu
akitolea mfano masaa kumi au zaidi kwa siku nivyema walipie kifurushi cha
shilingi 2500 cha siku nzima kwani kufanya hivyo inasaidia kulipa gharama
kidogo ukilinganisha na kulipa shilingi 500 kwa saa moja ambapo inakuwa gharama
kubwa zaidi.
Amesema
kwamba mteja atakaecheleawa kulipa ushuru anaodaiwa atatozwa faini ya shilingi
elfu kumi ndani ya siku 14,na kadri atakavyochelewa kulipa deni lake faini hiyo
itaendelea kuongezeka, hivyo wanaoegesha magari maeneo mbalimbali wanapaswa
kulipa ushuru wa maegesho kwa wakati ili kuepuka usumbufu.
“Kila baada
ya siku 14 endapo mteja ambaye amejisajili kwenye mfumo atakua hajalipa ushuru
wa maegesho anaodaiwa basi faini yake itaanza kuhesabika na endapo ataendelea
kukaidi kulipa atafikishwa kwenye vyombo vya Sheria kwa ajili ya hatua zingine
ambapo anaweza kufungwa jela mwaka mmoja
na kulipa faini pia kulipa deni lote analodaiwa “amesema Mkinga
Nakuongeza
kuwa “Nia ya serikali yakuongeza muda kutoka siku 7 hadi 14 isiwafanye wateja
wanaodaiwa ushuru wa maegesho isiwapelekee usumbufu hivyo watu wasitegemeee
kuulizwa na hakutakuwa majadiliano yoyote
ya ana kwa ana na mtoza ushuru,zoezi la kulipa kwa njia ya mtandao limeanza
rasmi Machi mosi mwaka huu.
Aidha sambamba
na hayo Meneja huyo amesema hatua za kuboresha mfumo huo zimefanikiwa kwa
asilimia 98 na TARURA bado inaendelea kuomba ushirikiano kwa wadau mbalimbali
ikiwemo vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya matumizi ya
mfumo huo.
Amesema
mfumo wa kielektroniki wa kukusanya ushuru wa maegesho ulianzishwa rasmi Mwezi
Septemba Mwaka jana ,lakini ulibainika kuwa na changamoto kadhaa ambazo baadhi
ya wateja walianza kuzilalamiki hata hivyo mwezi Oktoba 2021 serikali ilichukua hatua yakusitisha kwa muda matumizi
ya mfumo huo ili kuufanyia marekebisho.
Mwezi Machi Mwaka huu Mfumo huo umeanza rasmi kutumika baada ya kufanyiwa marekebisho makubwa ambapo changamoto zilizokua zimebainika ni pamoja na kukosekana kwa elimu yakutosha juu ya matumizi ya mfumo huo,pili wateja walioegesha magari kushindwa kufahamu wapi waliegesha magari yao,huku changamoto nyingine ikiwa ni kukosekana kwa taarifa zao za maegesho (Notefication) ambapo changamoto hizo tayari zimefanyiwa ufumbuzi.
No comments
Post a Comment