Jaji mlacha azindua kamati ya mawakili mkoa wa kigoma
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania
Kanda ya Kigoma Mhe. Jaji Lameck Mlacha(katikati) akifafanua jambo mbele ya
wajumbe Kamati ya Mawakili Mkoa wa Kigoma.
|
Na
Festor Sanga – Mahakama Kuu- Kigoma
Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania ya Tanzania Kanda ya Kigoma, Mhe. Jaji Lameck Mlacha
amezindua Kamati ya Mawakili Mkoa wa Kigoma,huku akiwataka wajumbe wa kamati
hiyo kufanya kazi kwa weledi na uadilifu.
Uzinduzi huo,
ulifanyika katika ofisi za Mahakama hiyo tarehe 02 Machi, 2022.
“Tendeni majukumu
yenu kwa mujibu wa sheria na msiende nje ya mipaka yenu” alisema Jaji Mlacha.
Aliwataka
wajumbe wa kamati hiyo kuhakikisha wanabuni njia za kuifanya ijulikane kwa Umma
ili wenye malalamiko dhidi ya wakili wajue pa kuyapeleka na kusema kuwa kamati
hiyo ijiweke kwenye nafasi ya ulezi wa mawakili.
Baada ya uzinduzi,
kamati hiyo ilianza kazi kwa kujengeana uwezo kwa kupitia sheria iliyoianzisha
(The written laws (Miscellaneous Amendments) (No.5) Act, 2021 na
kujua muundo na majukumu yake.
Akitoa mada katika
mafunzo hayo Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Kigoma, Mhe.
Gadiel Mariki ambaye ni Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema kuwa sheria
iliyoiunda ilianza kutumika rasmi tarehe 11 Oktoba, 2021 tangu ilipotangazwa na
Gazeti la Serikali na kuongeza kuwa kabla ya kuanzishwa kwa kamati hizo za
mikoa kulikuwepo na kamati moja tu ya kitaifa ikishughulika na mawakili wote.
Kutokana na idadi ya
mawakili kuongezeka kila mwaka, ililazimu kuanzishwa kwa kamati hizo za mikoa
ili kuratibu na kusimamia maadili na mienendo ya mawakili katika maeneo husika.
Kwa mujibu wa sheria
hiyo wajumbe wanaounda kamati hiyo ni pamoja na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu
ambaye ni Mwenyekiti, Wakili wa Serikali au Mwendesha Mashtaka wa Mkoa na
Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili(Chapter Convener) ambao ni wajumbe.
Aidha sheria hiyo
inaitaka kamati hiyo kuteua Afisa yeyote mwenye taaluma ya sheria ambaye
atakuwa Katibu wa Kamati. Kwa kuzingatia kifungu cha 4 A (2) cha sheria hiyo
kamati ilimteua Mhe. Anna Kahungu kwa Katibu wa Kamati.
Aidha, Kamati hizo
za Mikoa zinapaswa kutuma taarifa ya Utendaji kazi za kila robo mwaka kwa
Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
No comments
Post a Comment