WAZIRI MBARAWA ATOA MAAGIZO TRC
|
Na Mussa Augustine. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Makame Mbarawa
ameiagiza Bodi ya Wakurugezi ya Shirika la Reli Nchini (TRC)
kuhakikisha inasimamia kwa uzalendo utengenezaji wa Mabehewa ya Treni
iyendayo kwa kasi (SGR) ambayo yatatengenezwa na Kampuni kutoka China
inayofahamika kama CRRC inaternational. Waziri Mbarawa ametoa maagizo hayo Jijini Dar es
Salaam wakati wa kutiliana saini mkataba wa mwaka mmoja wa utengenezaji wa
mabehewa yapatayao 1430 yatakayogharimu dola za kimarekani milioni 127.2 sawa
na fedha za kitanzani kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 300. Aidha amesema kwamba utengenezaji wa mabehewa hayo
unapaswa kukamilika katika muda uliopangwa kwa mujibu wa Mkataba ,nakwamba
Bodi ya Wakurugenzi pamoja na timu itakayoenda nchini China kukagua
utengenezaji huo inapaswa kuhakikisha mabehewa hayo yanakua na ubora
unaotakiwa. " Huu mradi unatakiwa ukamilike kwa muda
uliopangwa naomba nitoe maagizo kwenu Bodi ya Wakurugenzi wa TRC na timu ya
watu mtakaoenda china kuangalia utengenezaji wa mabehewa haya kuhakikisha
mnafanya kazi hiyo kwa uzalendo,mabehewa yawe na kiwango cha ubora
unaotakiwa,pia msikubali eksichuzi zozote tunataka mradi huu ukamilike kwa
haraka ili ujenzi wa reli unapokamilika mabehewa yawe tayari"amesema
Waziri Mbarawa. Nae Meneja Mkuu Msaidizi wa Kampuni ya CRRC
International Tang Yun Peng ameihakikishia TRC kufanya kazi hiyo kwa
kuzingatia makubaliano yakimkataba yaliyosainiwa huku akiipongeza
Tanzania kwamba endapo mradi wa SGR utakamilika utafungua milango yakiuchumi
kwa nchi zingine za africa Mashariki. |


No comments
Post a Comment