JATU PLC YASAINI MKATABA WA MIAKA MITATU NA MRISHO MPOTO
Na Mussa Augustine
Kampuni ya JATU PLC inayojishughulisha na Kilimo imemteua rasmi kwa mara nyingine balozi wake Msanii Mrisho Mpoto kuwa Balozi wa Kampuni hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu nakwamba imemuandalia kipindi maalumu kiitwacha " Kaa Hapa Awamu ya Pili ) ili kuendelea kutangaza miradi mbalimbali ya Kilimo,Ufugaji,Maji,Ujenzi na Utalii.
Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa kutiliana saini na Msanii huyo Meneja Mkuu wa Kampuni ya JATU PLC Mohamed Simbano amesema kuwa uamuzi huo umekuja baada ya Serikali februari 7 mwaka huu,kumteua Mrisho Mpoto kuwa Balozi wa Wazara ya Maji kutokana na kutambua umuhimu wa Maji katika sekta ya Kilimo.
Aidha amesema kwamba Jatu imeamua kuunga mkono jitihada za serikali kwa kumteua msanii huyo ili kuendelea kutangaza miradi mbalimbali ya kilimo, Ufugaji ,Maji,Ujenzi,na Utalii,inayofanywa chini ya uongozi wa rais Samia Suluhu Hassan.
"Kwetu sisi sekta ya Maji ni Moja ya Nguzo muhimu sana katika kuleta mapinduzi ya Kilimo,hasa kilimo cha Umwagiliaji ambacho tumekua tukifanya katika mikoa mbalimbali ndani ya miaka mitano tka kuasisiwa kwa kampuni ya JATU PLC kwakweli tunakila sababu ya kujivunia na kutembea kifua mbele tukiwa kama vijana tuliothubutu kwa kuishi ndoto zetu kwa kufanya kazi kwa vitendo na kisha kuaminiwa na kulelewa na serikali kwa kipindi chote cha miaka mitano"amesema Simbano.
Aidha aemendelea kufafanua kua JATU PLC pamoja na kukumbwa na changamoto za hapa na pale lakini imefanikiwa kuingiza kampuni katika soko la hisa la DSE, kufungua ofisi kikanda ndani ya nchi na afrika mashariki kwa kuanza na Kenya kwa ajili ya kupanua wigo wa masoko ya ndani na nje,kufungua Kampuni ya Bima ya Kilimo na Ufugaji ,Ongezeko la Wakulima zaidi ya elfu tano.
Vilevile amesema mafanikio mengine kutoa ajira rasmi miatano na zisizo rasmi zaidi ya elfu kumi,kuchochea maendeleo ya Taifa kwa kulipa kodi mbalimbali pamoja na kukuza kipato kwa wanachama wake kwa kufanikiwa kuweka maigumo wezeshi na kuweza kufanya uwekezaju wa pamoja kupitia kampuni ya umma ya JATU PLC kwani asilimia 95 ya kampuni hiyo inamilikiwa na watanzania.
Kwa upande wake Mrisho Mpoto amesema hataiangusha kampuni hivyo atafanya kazi kubwa yakutoa elimu kwa jamii kutambua umuhimu wa Sekta ya Maji katika shughuli mbalimbali kama vile Kilimo, ambapo amesisitiza kwamba serikali imetilia mkazo mkubwa katika utekelezaji wa miradi ya maji nchini ikiwa lengo ni kumtua mama ndoo kichwani
"Naishukuru Serikali tarehe 7 kuniteua kua balozi wa Wizara ya Maji,lakini baada ya hapo tu JATU leo tarehe tisa mkaniteua kwa mara nyingine kuwa balozi wenu kwa mkataba mkubwa wenye heshima kubwa, nawahidi sitawangusha,nitatumia kipindi cha Kaa Hapa awamu ya Pili kupitia Chaneli 10 siku Jumatano Saa nne Usiku,na Marudio yake Jumanne saa tano Usiku ili kutoa elimu kwa watanzania kujua umuhimu wa sekta ya Maji" amesema Mpoto
Serikali imetilia mkazo sana katika sekta ya Maji,Mfano fedha za msaada za Uviko 19 serikali imetenga silimia kumi ya fedha hizo ambayo sawa na Bilioni mia moja thelathini na tisa na milioni mia nane ( 139.8) nakupelekwa sekta ya Maji ambapo ndio sekta pekee iliyopewa fedha nyingi,najua watanzania wengi hawajui hilo lakini hiyo ni kazi yangu ya kuelimisha naenda kuifanya " amesisitiza Mpoto.
No comments
Post a Comment