Zinazobamba

SERIKALI YATOA MAELEKEZO SITA KWA WAWEKEZAJI WA SEKTA YA MADINI

 




Na Mussa Augustine

Serikali imeagiza mambo sita kwa wawekezaji wa katika sekta ya Madini Nchini ikiwemo kuzingatia uhifadhi wa Mazigira na kutokujihusisha na utoaji wa ajira kwa Watoto Migoni.

Maagizo hayo yametolewa na Makamu wa Raisi Dr.Philip Mpango wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa Kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya Madini Tanzania 2022.

Mkutano huo ambao una kaulimbiu “Mazingira wezeshi kwa Maendeleo ya sekta ya Madini Tanzania”umewakutanisha wadau wa uwekezaji katika sekta hiyo kutoka ndani na nje ya Nchi.

Dr. Mpango ametaja mambo mengine kuwa wawekezaji wenye ubia na serikali waharakishe utekelezaji kwa mujibu wa makubaliano  ili wananchi waanze kunufaika.

“Suala la uharibifu wa Mazingira nina wakumbusha wachimbaji wote wakubwa na wadogokuzingatia sheria za mazingira ,wawekezaji wote mnawajibu wa wakuhakikisha shughuli zenu za uchimbaji,uchenjuaji,uchakataji wa madini zinatekeleza kwa mujibu wa sheria  na taratibu” amesema  Dr.Mpango

Aidha Makamu huyo wa rais pia amewataka wawekezaji wote hususani wakubwa wazingatie matakwa yatokanayo na tathmini ya athari kwa mazingira na jamii kwa kuzingatia misingi ya uzalishaji endelevu ,matumizi na mbinu bora za uzalishaji wa teknolojia bora na rafiki kwa Mazingira.

Ambapo jambo lingine amezikumbusha kampuni zote za uwekezaji katika sekta ya Madini zihakikishe zinatekeleza ipasavyo Matakwa ya kisherika ya kuandaa mipango ya ufungaji migodi na kuweka hati fungani ya urekebishaji wa mazingira.

Hata hivyo amezitaka Benk na taasisi zingine za fedha kushirikiana na shirika la Madini (STAMICO) kubuni namna bora zaidi ya kuwaqwezesha wachimbaji wadogo wakati serikali ikiendelea kuzifanyia kazi suala la kuanzishwa kwa benki maalumu ya madini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Madini Jonh Bina ametaja baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo kuwa ni pamoja na mitaji ambapo taasisis za fedha hutoa mikopo kwa wawekezaji wa uchimbaji dhahabu nakuwaacha kuwasaidia wendine.

Nae Waziri wa Mdini Dotto Biteko amesema uwekezaji mkubwa unaondelea kwenye utafiti wa Madini  maeneo mbalimbali ni uthibitisho tosha wa dhamira ya serikali ya kuwekeza katika sekta hiyo muhimu.

No comments