Zinazobamba

Naibu Waziri Atupele Kuunda Timu ya kushughulikia Changamoto Tazara


Na Mussa Augustine.

 Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete amesema kuwa Wizara yake itaunda Bodi Maalumu ambayo itakua inashughulikia changamoto mbalimbali zinazolikumba shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) ili kulifanya lifanye kazi zake kwa ufanisi mkuwa.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam wakati alipotembelea shirika hilo nakufanya mazungumzo na na watendaji na wafanyakazi wa shirika hilo pamoja na kukagua kalakana ya kukarabatia vitu mbalimbali ikiwemo injini na mabehewa.

Aidha Naibu Waziri Mwakibete amesema kuwa shirika hilo linakumbwa na changamoto malimbali ikiwemo Uchakavu wa Miundombinu , madeni makubwa ya wafanyakazi hali ambayo inachangia shirika hilo kushindwa kujiendesha kwa ufanisi mkubwa.

Pia amendelea kusema kuwa serikali ya Tanzania na Zambia zimeanza kufanya mchakato wa kubadilisha sheria ili kufanya marekebisho kwani sheria iliyopo kwa sasa inazuia kufanya uwekezaji wowote upande wa Tanzania bila kukubaliana na serikali ya Zambia.

“Tunashindwa hata kuendeleza upande wetu wa serikali kwasababu sheria iliyopo inazuia kuwekeza chochote katika reli hii mpaka tukubaliane na wenzetu hivyo tayari mchakato wa kubadilisha sheria hii unaendelea tukikamilisha hata baadhi ya changamoto zitapungua”amesema Naibu Waziri huyo.

Aidha ameongeza kuwa baadhi ya Wafanyakazi wa TAZARA hawapewi mikataba ya kudumu ya ajira hali ambayo inawafanya wakose morali  ya kufanya kazi huku akisema kuwa suala hilo linafanyiwa kazi na serikali.

 

 Kwa upande wake Meneja Mkuuu wa TAZARA Tanzania Fuad Abdallah amesema kwamba shirika hilo linakumbwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchakavu wa Miundombinu,upungufu wa mabehewa na injini ,Madeni ya wafanyakazi,Madeni ya Mifuko ya Kijamii,pamoja na Madeni yawasanbazaji .

“Shirika hili lmanzishawa mwaka 1976 ni miaka kama arobaini na mbili sasa lilianzishwa likiwa na injini 106 lakini kwa sasa tuna injini 14 pekee,ni changamoto tunaupungufu mkuwa wa inji na mabehewa “amesema Abdallah.

 

 

No comments