WAZIRI MKUU ATOA TUZO YA KISWAHILI KWA WASHINDI WA MWAKA 2021
|
Na. John Mapepe Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Kassim Majaliwa Majaliwa leo Januari 27, 2022 ametoa Tuzo ya Kiswahili ya Mabati -Cornell ya Fasihi ya Afrika kwa washindi wa mwaka 2021 jijini Dar es Salaam.
Katika kundi la Riwaya Halfani
Sudy ameibuka kuwa mshindi wa kwanza, Mohamed Omary ameibuka mshindi wa
kwanza kundi la shairi, wakati Mbwana Kidato ameibuka mshindi wa pili
katika kundi la tamthilia na Lukas Lubungo kuwa mshindi wa pili kwenye
kundi la hadithi za kubuni. Amesema dhamira ya
Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo ya kutekeleza mkakati
wa kubidhaisha lugha ya Kiswahili Kitaifa na Kimataifa, ambao utazinduliwa
hivi karibuni itafanikiwa ikiwa wadau wote watajitoa kwa dhati kutekeleza
mkakati huu na kusimamia maendeleo ya lugha hii adhimu na aushi.
Mhe. Majaliwa amezipongeza
kampuni za SAFAL na ALAF kwa kufadhili tukio hilo na ametoa wito kwa
makampuni mengine kuiga mfano huo kwa kuwekeza katika lugha hiyo, huku
akisisita kuwa kuwekeza katika Kiswahili itakuwa ni njia mojawapo ya
kurudisha fadhila kwa wananchi ambao ndio wateja wa bidhaa hiyo.
Aidha, Mhe
Majaliwa amesema Kiswahili kimetambuliwa kimataifa kwa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kutangaza tarehe 7
mwezi Julai, kila mwaka kuwa Siku ya Kiswahili Duniani ambapo ameitaka
Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuanza kuandaa wiki ya maadhimisho ya
kiswahili katika siku ya mwaka huu.
Mhe. Majaliwa ametumia muda
huo kutoa maelekezo mbalimbali ya kukuza lugha ya kiswahili kwa vyombo vya
Serikali vinavyojihusisha na lugha ya kiswahili.
Naye, Waziri wa
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Wizara yake
itashirikiana na wadau mbalimbali kukuza lugha ya kiswahili ili kufika sehemu
mbalimbali duniani.
Mhe. Mchengerwa
ameelekeza wadau mbalimbali wa lugha ya hiyo kuhakikisha
wanaisherekea kwa namna ya pekee siku ya kiswahili ya Julai 7 mwaka huu
kwa namna ya kipekee ili kuthibitishia dunia kuwa Tanzania ndiyo
chimbuko la lugha hiyo.
Katika halfa
hiyo, Waziri Mkuu Mhe Majaliwa na Mhe. Mchengerwa walitumia nafasi
hiyo kumtakia heri ya kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Samia Suluhu Hassan kwa wimbo wa kiswahili wa heri ya kuzaliwa ulioongwazwa
na jaji mkuu wa tuzo hizo Profesa Aldin Mutembei kutoka Chuo Kikuu cha
Dar es Salam.
|
No comments
Post a Comment