Brela yapata mwitikio mkubwa Mliman city, Wafanyabiashara ‘bubu’ wapewa rai
| Afisa leseni na biashara wa Brela, Bi. Sada Kilabura akizungumza na mteja alifika Mliman City Kupata huduma. |
| Afisa leseni wa Brela, Bw. Robert Mashika akizungumza na wateja. Mashika amesema zoezi la usajili limeitikiwa vizuri na kwamba anaimani mpaka siku ya kufunga jioni watu wengi watakuwa wamefikiwa. |
| Afisa leseni Robert Mashika akizungumza na Kituo cha Redio Imaani iliyopo mjini Morogoro kwa kutumia njia ya simu, wasikilizaji wa kituo hicho walipata bahati ya kupata elimu juu ya huduma za Brela. |
| Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupatiwa huduma Mliman City. |
Na Suleiman Magali
Ikiwa leo ni sku ya pili toka
kuanza kwa maonyesho ya siku tano ya utoaji huduma za Brela katika Parking za
Mlimani City Jijini Dar es salaam, imeelezwa kuwa mwitikio wa wananchi umekuwa
mkubwa ukilinganisha na siku za awali.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi, Afisa leseni wa Wakala wa usajili wa Biashara (Brela), Bw. Robert
Mashika amesema zoezi la usajili limekwenda vizuri kwani Zaidi ya wananchi 200
wamefanikiwa kupata huduma ikiwamo usajili wa majina ya Kampuni pamoja na
kusikilizwa
Mtaalam huyo wa masuala ya
leseni amesema mbali na idadi hiyo ya wananchi waliofanya jitihada za kufika
viwanja vya Mlman city na kusikilizwa lakini pia dalili zinaonyesha kutakuwa na
ongezeko la watu hapo siku za usoni kabla ya kumaliza maonyesho yao siku ya
jumapili.
Fullhabari ambayo
ilifika viwanja vya Mliman City Mapema ilishuhudia Wananchi wakipatiwa huduma,
huku wengine wakipatiwa vyeti papo kwa papo.
Huduma ambazo zimekuwa
zikitolewa viwanjani hapo ni pamoja na usajili wa Nembo ya Biashara,
hataza, hati vumbuzi na usaidizi wa kujaza taarifa katika mtandao.
Aidha amewataka wananchi wote
hususani wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na viunga vyake kuchangamkia fursa
hiyo ili kupata majibu ya maswali yao na ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili
zikiwemo mifumo ya mtandao.
Wananchi wasifu ubunifu, watoa rai
Wakizungumza na vyombo vya
habari mmoja wa wananchi aliyejitokeza uwanjani hapo Bw. Ramadhani Mmanga
ametoa rai kwa wafanyabiashara wengine kuhakikisha wanasajili biashara zao ili
wafanye kazi kisheria.
Naye Mohammed Mseja ambaye alifanikiwa kusajili Biashara yake na
kupatiwa cheti chake papo kwa hapo hakusita kuonyesha furaha yake hasa baada ya
kupata cheti chake.
.
Pia Mseja ameungana na Mmanga
kuwashauri wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza katika viwanja vya mliman City
ili kusajili biashara zao ili waweze kunufaika na mbambo mbalimbali
Ends,
No comments
Post a Comment