Brela yawaita wana-Dar es salaam Mliman city, wapiga kambi siku tano
| Afisa Tehama wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Joram Manyika akiwa katika viwanja vya Mliman City tayari kwa kutoa huduma |
Na Suleiman Magali
Wakala
wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imetoa wito kwa wakazi wa Dar es salaam kutumia fursa
ya maonyesho ya siku 5 yanayofanyika katika ukumbi Mliman City, kujitokeza kwa
wingi ili kupata usaidizi wa changamoto wanazokumbana nazo kwenye kusajili
biashara zao.
Wito
huo umetolewa na afisa leseni na biashara wa Brela, Bi. Sada Kilabura jana,
Januar 26, 2022 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari
viwanjani hapo.
Alisema maafisa wa wakala wamejipanga vizuri
kuwahudumia wananchi na kwamba hawatatumia muda mwingi kupata huduma.
“Kw
majina naitwa Sada Kilabura, Afisa leseni kutoka Brela, tumeandaa maonyesho
haya ili kutoa elimu kwa umma kuhusu huduma zinazotolewa na Brela, tunatoa
huduma za kuandikisha majina ya biashara, Kampuni, alama ya biashara na huduma.
Pia
tunatoa leseni za viwanda pamoja na kutoa leseni za biashara kwa daraja A,
maonyesho haya ni fursa kwa wakazi wa Dar es Salaam kufika na kupatiwa huduma
hasa kwenye changamoto zao wanazokumbana nazo.
Tupo
hapa kwa siku 5, kuanza Januari 26 hadi 30, 2021, Nitowe wito kwa wafanya
biashara wote, wadogo na wakubwa, waliosajiliwa na ambao bado hawajasajiliwa, wajitokeze
Mlimani City.
“Inawezekana
kabisa kuna baadhi ya wateja walisajiliwa kwa njia ya makaratasi, sasa hivi
wanatakiwa kuhuisha taarifa zao kwa njia ya mtandao, hapa ndio sehemu sahihi ya
kuja kupata usaidizi.
Aidha
alisema kwa wale ambao bado hawajajiunga na huduma ya mmiliki mwenye manufaa
(Beneficial owneship), tunawaomba wafike hapa kupata usaidizi.
Aidha
kwa upande wao wananchi waliohudhuria maonyesho hayo wamesifu huduma
inayotolewa na maofisa wa Brela, wakisisitiza kuwa wanawapokea vizuri na
kutatua kero ambazo wanakumbana nazo katika kuhuisha taarifa zao.
“Huduma
tulizopatiwa hapa Mliman City ni nzuri, zimejaa upendo, nawashauri wale wenye
nia ya kuanzisha Kampuni/ au kusajili majina ya biashara yao wasisite kufika
Mliman City kupata huduma,” alisema Marco
Aidha
Marco Luena ameongeza kusema kuwa
aliwahi kupata shida kwenye kujaza taarifa zake katika mtandao lakini alipofika
Mliman City maafisa wa Brela walimsaidia.
Naye
Frank Mambali kutoka Ilala amesema ili kufanikiwa katika biashara ni lazima isajiliwe,
changamoto kubwa aliyokuwa akiipata ni jinsi ya kuwafikia maafisa wa Brela,
kwani mara nyingi wakifika ofisini kunakuwa na foleni za wateja, lakini kitendo
chao cha kuamua kutoka ofisini na kuwafuata wateja waliko kinasaidia sana
kuharakisha michakato ya usajili.
BRELA
inatoa huduma mbalimbali zikiwemo usajili wa majina ya biashara, usajili wa
alama za biashara na huduma, usajili wa makampuni, kutoa hataza kwa maana ya
hati miliki kwa vumbuzi ambazo zinasaidia kutatua changamoto katika jamii”.
No comments
Post a Comment