Zinazobamba

MEYA KUMBILAMOTO AZINDUA KIWANDA KIDOGO CHA KUCHAKATA TAKA KUWA MKAA CHA SAUTI YA JAMII KIPUNGUNI.

Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto ametoa ahaadi ya kutoa msaada wa Vyerahani kwa ajili  Sauti ya Jamii Kipunguni Wilayani Ilala.

Meya wa jiji la Dar es salaam Mh. Omary Kumbilamoto akizindua kiwanda kidogo cha Sauti ya Jamii Kipunguni
Meya Kumbilamoto alitoa ahadi hiyo Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa Kiwanda cha kuzalisha  Mkaa  Kilichofadhiliwa na AMREF   Kimeligharimu shilingi milioni 26.

Akizindua mradi huo wa kisasa Meya Kumbilamoto aliwataka Sauti ya Jamii kutunza mradi huo wa kisasa na kuendeleza kwa ajili ya kutunza mazingira .

"Ninajivunia ndani ya Halmashauri yetu ya Ilala Kituo cha Taarifa na Maarifa kwa mafanikio makubwa walioyapata Sauti ya jamii kipunguni mmekuwa wabunifu wakubwa katika kubuni shughuli za kijamii ikiwemo Kilimo na chuo cha ushonaji 
natoa ahadi yangu nitawaletea vyerahani kwa ajili ya kikundi chenu vijana waweze kujifunza pamoja na feni "alisema Kumbilamoto.

Kumbilamoto alisema kuhusu mradi wa mkaa aliozindua changamoto zilizoelezwa katika mradi huo waandike barua walete ofisini ofisi ya Meya itasaidia kwa ajili ya maendeleo ya Wilaya ya Ilala.
Alisema SAUTI ya JAMII Kipunguni mmekuwa chachu ya maendeleo katika mafaniko yenu sambamba na kuisaidia serikali .

Wakati huohuo Meya Kumbilamoto amemwagiza Afisa  Maendeleo Wilaya kuelekeza mikopo kata ya Kipunguni ikiwemo kikundi cha Sauti ya Jamii ambapo ina miliki mradi mkubwa na kutoa elimu kwa jamii.

Naye Mkurugenzi wa TGNP Lilian Liundi alisema TGNP wanajivunia sana na Sauti ya Jamii Kipunguni kwa wilaya ya Ilala imeweza kuleta mafanikio makubwa kupitia kituo chao cha Taarifa na Maarifa katika kutoa elimu kwa jamii na kukemea vitendo vya ukatili.

Ameendele kwa kusema kuwa anatarajia kuona vitu vingi zaidi ya hicho kiwanda kwani anatamani siku moja kipunguni ijekuwa na sehemu kubwa inayozalisha vitu vingi na kuweza kutoa ajira kwa vijana wengi zaidi hapa nchini.

Ameongeza kuwa wao kama walezi wanajivunia kuona kituo hicho kinatandaa na kufahamika sehemu nyingi kufikia kupata wadau wengi wanaokifadhili hicho, kwa  fedha elimu na njia nyingine zote zitakazoweza kuleta faidha kwa kikundi hicho na taifa kwa ujumla.

Kwa upande Mwenyekiti wa  Mtaa huo Danieli Malagashimba alisema kiwanda hicho  ni  matokeo ya Mheshimiwa Diwani mstaafu Mohamed Msofe akishirikiana na Mwenyekiti  Malagashimba wamekuwa  walezi na wadhamini wa Sauti jamii kipunguni toka  mwaka 2016 mpaka sasa.

Malagashimba alisema  Taasisi ya Sauti ya Jamii  imekuwa kufikia uanzishwaji wa kiwanda kupitia wadau wafadhili AMREF,TGNP na WILDAF ambapo alisema lengo la kiwanda hicho cha kuzalisha mkaa kutoa ajira 300 kwa Wanawake na Vijana  na kuendeleza usafi wa mazingira kwa kuzalisha nishati ya mkaa .

Alisema  awali alishawawezesha Sauti ya Jamii Kipunguni vyerahani viwili ambavyo vinatumika ambapo alisema kiwanda hicho cha kisasa kipo katika mtaa wake kitawawezesha vijana kujikwamua kiuchumi  katika kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan

Kipunguni uzinduzi  wa Mradi wa Kiwanda cha kuzalisha mkaa 
January 22/2022
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Lilian Liundi akiongea na wakazi wa kata ya Kipunguni ambao hawapo pichani, katika Uzinduzi wakiwanda kidogo cha Sauti ya Jamii.
Mwenyekiti wa mtaa wa Amani Mh. Daniel Malagashimba akitoa neno katika uzinduzi wa kiwanda kidogo cha kutengenezea mkaa mbadala cha Sauti ya Jamii Kipiunguni.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Kipunguni wakifuatili zoezi la uzinduzi wa kiwanda kidogo cha kuchakata takataka kuwa mkaa kilichopo Kipunguni jijini Dar es salaam.

Viongozi mbalimbali walioudhuria zoezi la uzinduzi wa kiwanda cha Sauti ya Jamii, wakipokea cheti kwa niaba ya kituo cha Sauti ya Jamii kilichotolewa na SIDO.

No comments