Zinazobamba

Wananchi: Brela imebadilika, tunaomba wafike na mikoani

Afisa leseni Robert Mashika akisikiliza kwa makini wateja waliofika kuhudumiwa.



Afisa Tehama wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Joram Manyika akizungumza na wateja katika viwanja vya Mlimani City


 



Na Suleiman Magali

Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wamesema Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wanaonekana wameanza kubadilika kutoka kufanya kazi kwa mazoea na kuamua kuwafuata wananchi waliko kutatua kero zao.

Wakizungumza na Fullhabari Blog baadhi ya wananchi waliofika viwanja vya Mlimani City wamekili kuona mabadiliko ya huduma na kuamua kutoa kongole kwa Mkurugenzi wa wakala kwa namna alivyoweza kuibadilisha.

Mmoja wa wananchi waliotoa pongezi kwa wakala wa leseni na biashara ni Omar Abdallah ambaye amesema watu wengi walikuwa na mtizamo hasi na wakala lakini alivyofika Mliman city amejionea huduma ya viwango vya kimataifa.

“Unajua kuna watu walikuwa wanasema Wakala wa leseni Brela haipigi hatua kwa sababu ya watendaji kuwa na tabia isiyofaa (Negative attitude), lakini sasa wanaonekana wamebadilika na ndio maana wananchi wengi wamehudhuria.

Aidha, wametoa rai kwa wakala kuhakikisha inaendelea kutoa elimu nchi nzima kuhusu huduma zao kwani watu wengi bado wanakwama katika kutumia mifumo ili kujisajili.

Wamesema kupitia mwanya huo (gap) watu wengi wamekuwa wakipigwa (wakiibiwa) na vishoka.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa cheti chake Armani Dior ameiomba BRELA kuongeza Elimu kwa wananchi juu ya kutumia mifumo ya mtandao ili kuepukana na vishoka.

“Naiomba sana BRELA watusaidie kutoa  elimu, hapa ukiangalia wengi walijaribu kusajili kwenye mtandao lakini kuna mahali walikwama, matokeo yake wale vishoka wanapata nafasi ya kufanya Biashara" amesema Dior.

Vilevile amesema Wakala ukiamua kwenda mikoani utasaidia watu wengi kutimiza ndoto za kusajili biashara zao.

Aidha amewahimiza wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kutumia fursa hiyo kupata elimu itakayosaidia kuepukana na vishoka wa mitaani. 

Wakala wa leseni na Biashara Brela umeendelea na zoezi lake la kukutana na wananchi mbalimbali kwa Lengo la kutatua changamoto zinazowakabili.

Katika siku ya leo Januari 28, 2022 jumla ya Majina ya Biashara 26 na Makampuni 7 yalisaliwa na baadhi yao kufanikiwa kupatiwa vyeti vyao pao kwa hapo.

BRELA bado wapo kwenye viwanja ya Mlimani City, wanatarajia kufika tamati Jumapili, Januari 30, 2022

No comments