Zinazobamba

"Mbinu za kufanikiwa kimaisha ni kuwekeza katika kujisomea vitabu mbali mbali vya ujasiliamali" - Dk Dornald Olomi

IMEELEZWA kuwa mbinu za kufanikiwa kimaisha ni kuwekeza katika  kujisomea vitabu mbali mbali vya ujasiliamali na sio kuwekeza  katika elimu ya darasani pekee.


Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji katika taasisi ya Uongozi na Ujasiliamali (IMED) Dk  Dornald Olomi, wakati wa uzinduzi wa kitabu  kiitwacho   Anza Kuwa na Stawi.

Dk  Olom alikuwa Mgeni rasmi katika uzinduzi wa kitabu hicho kilichoandikwa na Prosper Lemmy Magali, ambaye ni  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wadau wa Nishati  Jadilifu  Tanzania( TAREA), pia ni Mkurugenzi  wa Ubunifu na   Uendelezaji mradi wa Ensol (T) Ltd.

Dk. Olomi ambaye pia yupo katika kamati  ya taifa katika maendeleo ya elimu nchini, alisema kazi ya kuboreshwa mitaala bado inafanywa ambapo mwaka 2015  mitaala katika topic zimeishawekwa  kwa wanafunzi kuanzia darasa la tatu na kuendelea kusoma masuala ya ujasiliamali.

 " Changamoto ipo katika suala la elimu ambapo wapo baadhi ya wanafunzi wanamaliza darasa la Saba hawajui kusoma na kuandika,_ alisema.

Aliongeza kuwa inatakiwa kuwe na shule za mfano ambazo wanafunzi watafanya kitu na kitaonekana.

Akizungumzia masuala ya biashara alisema biashara mtu anaanza na mtaji mdogo na baadae anafika mbali kibiashara.

Alisema kuwa mbinu za kujifunza kukuza ujasiliamali ni kujifunza kusoma vitabu mbalimbali vya ujasiliamali.

" Nchi imepiga hatua baada ya kuwasaidia watu njia mbalimbali  za ujasiliamali ," alisema.

Aliongeza kuwa nafasi ya familia  katika malezi inatakiwa vijana wajengewe uwezo katika masuala la ujasiliamali.

Akizungumzia mfumo wa kisera na Sheria, alisema kuwa 
mfumo wa kisera na kisheria  uwepo kwa ajili ya kusimamia biashara  zilizokuwa TIN.

Alisema  kwanza mtu anatakiwa awe na kumbukumbu katika biashara zake, awe mwelewa katika ulipaji wa kodi pia  kuna mbinu zinatakiwa kuangaliwa ili mtu aweze kulipa Kodi.

Magali alisema kuwa kuandika kitabu hicho na kikisomwa kutawasaidia watu mbalimbali kubadilika kimaisha .

Alisema takwimu zinaonyesha asilimia 70 ndio walioajiliwa katika sekta binafsi .
Aliongeza kuwa watu wanamaliza vyuo, lakini hawana ajira rasmi, pia kundi kubwa la watu  halipo katika  sekta  yoyote rasmi na ni hao wanaochangia uchumi  wa nchi kwa asilimia kubwa .

" Ili kupunguza tatizo la ajira  ni lazima kuwasaidia waweze  kukuwa na uthubutu ," alisema.

Aliongeza kuwa wafanyabiashara na wajasiliamali  ambao Sasa ni  wakubwa katika biashara zao  walianza kwa biashara ndogondogo  leo niwafanyabiashara wakubwa.," alisema..

Aliongeza kuwa  inatakiwa kukuza vipaji vyao ili waweze kunufaika na fulsa zilizopo.

Rashid Hamza Nzowah  ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji kutoka Gereji ya Nzowah anasema Siri ya mafanikio yake ni uhaminifu katika kazi za wateja wake.

Anasema mtu akiwa muaminifu anapata wateja mbalimbali ambapo watafika kupata huduma kwake.

" Nimekuwa mwaminifu, pamoja na kuwa na watumishi katika kampuni yangu, Mimi nafanya kazi za kampuni yangu hata nikipigiwa simu usiku wa manane naenda kufanya kazi, anasema.

Rashid anasema alianza kujifunza ufundi Gereji mwaka 1996, pamoja na kujifunza ilipokuwa ikifika mida ya jioni anakwenda kusoma VETA masuala ya ufundi.

Anaongeza kuwa baada ya kumaliza masomo VETA   aliweza kufungua Gereji yake iitwayo Nzowah iliyopo Ilala Jijini Dar es Salaam na kuajili vijana 18.

Anasema  Gereji yake imesajiliwa na ipo katika ubora wa Gereji 20 zilizopo hapa nchini.

"Gereji yangu imesajiliwa niya kisasa Gereji Kati ya Gereji 20 za Tanzania zilizo bora nami Gereji yangu IPO," anasema.

Anaongeza kuwa  katika Gereji Bora 20 zilizopo Tanzania huwezi kuacha kuitaja Nzowah .

 Anasema uaminifu wake katika kazi umemfanya  aaminiwe na taasisi mbalimbali na mashirika, makampuni.

Anasema uaminfu wake umemfanya afanye  kazi zake kwa weledi na kufanikiwa kutoa huduma za Gereji maeneo mbalimbali.

Anasema anatarajia kuendelea kutoa huduma hiyo katika maeneo mbalimbali ya nchi.


No comments