Zinazobamba

SHULE YA MOUNT KIBO ILIYOPO MBEZI BEACH JIJINI DAR ES SALAAM YAADHIMISHA MIAKA 25 TANGU KUANZISHWA KWAKE

Na. Mussa Agustine

Katika Kusherehekea maadhimisho ya miaka ishirini na tano tangu kuanzishwa kwa shule za Awali na Msingi Mount Kibo, shule hiyo imewashauri Watanzania kupenda kuwasomesha Watoto wao katika shule za ndani ya Nchi ili kuiendeleza sekta ya elimu kwa Pamoja na kujenga Taifa la watu makini.

Nembo Inayoonesha miaka 25 ya shule ya Mount Kibo

Ushauri huo umetolewa na mkuu wa shule za Mount Kibo zilizopo Mbezi Beach Dar es salaam Gaudence Liganga wataki akizungumza na waandishi wa Habari waliotembelea shuleni hapo kujionea mafanikio iliyoyapata tangu kuanzishwa kwake mwaka 1996

Bwana Liganga amesema kwamba kasumba ya kuwapeleka Watoto kusoma shule zilizopo nje ya Nchi wengi wao hurudi wakiwa wamepoteza maadili yao ya kitanzania nakuiga tabia za ugaibuni jambo ambalo linapelekea kukosa uzalendo katika nchi yao.

Aidha amesema kwamba Shule ya Awali na Msingi ya Mount Kibo imepata mafanikio makubwa ikiwemo kuwa na majengo yenye miundombinu ya kisasa kujifunza kwa Watoto,Usafiri wa uhakika kuwachukua na kuwarudisha wanafunzi,Mabweni ya kisasa,Viwanja vya Michezo.

Mafanikio Mengine  ya shule hiyo imefanikiwa kutoa ajira zipatazo 67 za walimu wa mahili katika ufundishaji ,huku nafasi za ajira Zaidi ya 50 za watumishi wasio walimu wakiwemo Madereva,Wapishi na nafasi zingine muhimu za Kazi.

“Ndugu wanahabari shule hii imenzishwa mwezi Novemba 1996, na muasisi wa shule hii mzee mstaafu Bwana Elia Urasa na Mkewe Bibi Doroth Urasa ikiwa lengo ni kutoa huduma ya elimu kwa watanzani,tulianza na wanafunzi tisa tu,kwasasa tuna wanafunzi 1200 na kati yao wanafunzi 300 ni wa awali na 900 ni Msingi ,kwa kuwa tunathamini vya kwetu shule imeajiri walimu wengi wa kitanzania” amesema Mwalimu Liganga.

Aidha Shule hiyo imeafanikiwa kushika nafasi ya 11 katika wilaya ya Kinondoni kwa matokeo ya Darasa la Saba ya m waka 2021, kutoka nafasi ya 19 kiwilaya mwaka 2020, huku imejiwekea malengo ya kuendelea kufanya vizuri kwa kutoa elimu bora Zaidi na kushika nafasi za juu Zaidi nakwamba inatarajia kuanzisha shule ya sekondari ambapo tayari eneo la kujenga shule hiyo lipo na wanamalizia taratibu za usajili wa shule hiyo ya sekondari.

Mwalimu Liganga ameendelea kufafanua kwamba katika kukuza vipaji shule hiyo imetenga siku ya Jumamosi kuwa siku ya Michezo na kuonyesha vipaji vya Watoto shuleni hapo,ambapo Watoto wengi wamekuwa wakionyesha vipaji vya michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa Miguu,Mpira wa Pete,Mpira wa Kikapu,Pamoja na Uimbaji na Upigaji wa Piano ,nakwamba uongozi wa shule hiyo unapogundua kipaji cha mtoto unamuita Mzazi au Mlezi na kujadili nae namna ya kuendeleza kipaji chake.

Hata hivyo kwa Mujibu wa Mkuu huyo wa Shule amesesma Shule hiyo imekuwa na mashirikiano makubwa ya kitaaluma na shule Jirani kwa kukutana wakuu wa shule kujadili namna ya kuendeleza elimu,kushirikiana katika mitihani ya ujirani mwema inayoandaliwa na shule hizo au taasisi mbalimbali za elimu.

Mkuu wa shule za Mount Kibo zilizopo Mbezi Beach Dar es salaam Gaudence Liganga akiongea na waandishi wa habari waliyotembelea shuleni hapo mapema leo.


Baadhi ya majengo ya shule ya Mount Kibo iliyopo jijini Dar es salaam.
Muonekano wa nje wa shule ya mount kibo.

Nembo ya shule ya mount kibo.

Hakuna maoni