Bi Fatma: Dereva Mlemavu anayetamani kumiliki benzi
Makala Maalum
Kuzaliwa mlemavu haimanishi kuwa
wewe ni tegemezi, uwe ni wa kusaidiwa tu, ulemavu ni mapungufu ya kimaumbile
mwanadamu anapaswa kuyakubali, gazeti imaani imefanikwa kukutana na mmoja wa
watu wenye ulemavu wa miguu ambaye amekataa kuwa tegemezi, akapambana na maisha
na sasa ni kama anaiona nuru, huyu haya Bi Fatma Amri Abdallah kutoka mkoani
Lindi akieleza jinsi alivyofanikiwa kuyakubali mapungufu yake ya kimaumbile na
kuamua kufanya kazi ya bajaji na kujiingizia kipato chake cha halali
Fullhabari: Tueleze kwa kifupi
wewe ni nani na historia yako kwa kifupi
Bi. FATUMA Amri Abdallah: Mimi ni
mama, nimezaliwa mwaka 1981, Mkoani Lindi, kama unavyoniona ni mlemavu wa miguu
yote miwili, ili nipate riziki yangu ni lazima nitambae kutoka sehehmu moja
kwenda nyingine, Nashukuru Mungu nimeolewa na mume wangu ananipenda ukweli wa
kunipenda, mimi na Mume wangu tumefanikiwa kupata mtoto mmoja. Pamoja na kuwa
katika ndoa na ulemavu wangu wa miguu, hali hii haijanfanya nibweteke. nimeamua
kujishughulisha na utafutaji wa riziki ya halali. Katika familia yangu mimi ni
mtoto pekee mwenye ulemavu, sikuzaliwa mlemavu, bali nlipata ulemavu nikiwa na
umri wa miaka mitatu, baada ya kuugua na kupelekea ulemavu wangu, kabla ya hapo
nilikuwa natembea kwa miguu yangu miwili kama wengine
Fullhabari: Tueleze kwa kifupi ni
kitu gani kilichokusukuma kuingia katika biashara?
Bi. Fatuma Abdallah: Nachukia kuwa tegemezi, mambo ya kuwa ombaomba sipend kabisa, najua maumbile yangu ni mtihani lakini siyo sababu ya kubweteka, nilikuwa naomba Mungu anisaidie nipate kuwa na uwezo wa kufanya kazi zangu mwenyewe katika njia inayompendeza. Nashukuru Mungu alinijibu, alinipitisha njia ambazo leo hii nimekuwa ni mtu wa kufanya kazi zangu mwenyewe. Kwa sasa mimi ni dereva wa usafiri maarufu wa Pikipiki za miguu mitatu, maarufu kama Bajaji, nipo hapa mtaa wa Kongo na uhuru, Kariakoo jijini Dar es Salaam, nabeba abiria kutoka hapa kwenda feri na posta. Nimejitosa kufanya shughuli hii ya usafirishaji kwa dhamira ya kujikomboa kiuchumi, kama unavyoona mtaa huu ni mtaa wenye kila aina ya vurugu, msongamano wa watu na magari mengi. Namshkuru Mungu nafanya kazi hizi nikiwa nimevaa hijabu/ Nikaab na wateja wangu wanakubali hali hiyo. Fullhabari ilimshuhudia Fatma akiwa katika vazi tukufu la Niqaab, akifunika mwili wake wote, ukimkuta katika kazi yake utaona macho yake tu lakini vingine vyote vimestriwa na vazi la hijab. Yaani huwezi kujua kama ni mlemavu
Fullhabari: Pengine kabla ya
kufanya kazi hii ya sasa uliwahi kufanya biashara? Kwa nini bajaji ya miguu
mitatu
Fatma Abdallah: Ndoto ya kuwa mfanyabiashara
imetoka mbali sana, nakumbuka nikiwa nasoma shule ya msingi, nilianza kufanya
kazi za mikono, nilianza kupika vitumbua, chapatti na maandazi, baadae nlipata
hamu ya kuondoka Mkoani Mtwara na kuja Jijini Dar es Salaam.
Lakini nilipomueleza mama yangu
mzazi nia yangu hiyo, mama alinikatalia na hakunipa sababu ya kunikatalia. Ila
nadhani mama yangu alikuwa anahofia kuwa mtoto wake nitajiingiza katika kazi ya
kuomba.
Nilimhakikishia mama yangu kuwa sitojiingiza
katika shughuli ya kuwa ombaomba.
Nilimjengea hoja mama yangu kuwa mimi
nina ulemavu wa miguu lakini Mwenyezi Mungu ameniachia akili na mikono katika
hali ya utimamu wake hivyo anaweza kujishughulisha na kazi mbalimbali na kuweza
kujipatia kipato halali.
Mama alinielewa na hatimae niliingia
Jijini Dar es Salaam, nikitokea Mtwara na kufikia kwa kaka yangu anaeishi Yombo
Buza, na baada ya muda nilimuomba kaka yangu mtaji ili nianze kujishughulisha
na biashara ndogo ndogo.
Bahati nzuri nlipata mtaji kutoka
kwa kaka yangu, nilianza kuuza saa na mikoba ya wanawake, kituo changu cha
kwanza kufanyia biashara hizo kilikuwa Karume Jijini Dar es Salaam.
Changamoto…
Siku moja nilienda kuswali
Msikiti wa Lindi, Kariakoo Jijini Dar es Salaam, wakati huo nikiwa natumia
Baiskeli za walemavu ambayo pia ilikuwa ikimsaidia kubeba bidhaa zake za biashara.
Nilipofika msikitini niliacha
mzigo wangu nje katika baiskeli yangu na kuingia Msikitini, kwa ajili ya
kufanya ibada lakini nilipotoka sikukuta mzigo. Yaani niliibiwa mikoba yangu
yote ya biashara.
Sijakata tamaa, hali hiyo iliniongezea
hamasa ya kutafuta zaidi, ilinibidi niende kwa jamaa mmoja wa Kihindi na
kumuelezea changamoto yangu ambapo aliniliza kama nitaweza kazi ya kuendesha
Pikipiki aina ya Bajaji.
Bila hofu na kwa kujiamini nikajibu
naweza na kwamba nipo tayari kufanya kazi hiyo.
Hata suala la kuwa na leseni
lilikuwa kama ni dalili ya kikwazo kwangu kupata neema ya ajira hiyo mpyao, ikanibidi
kwenda kujiunga na Chuo cha Ufundi, Polisi Kilwa Barabara ya Kilwa na kusomea
udereva na baada ya kuhitimu nilipata leseni ya kunihalalisha kufanya kazi ya
udereva barabarani kwa mujibu wa sheria.
Baada ya kuhitimu kozi hiyo ya
udereva na kurudi kwa Mhindi, Mhindi aliamua kuninunulia Pikipiki ya miguu
mitatu aina ya Bajaji na kusaini mkataba kwa makubaliano maalum ya kibishara.
Atoa wito…
Naomba niwatake wanawake
wasiogope kufanya kazi wakiwa katika stara, kwani kazi ni za muda mchache
lakini Stara ndio kila kitu.
Kumbuka utaenda kujibu nini mbele
ya Allah kwa kuacha stara kwa ajili ya kazi, ikibidi ifike mahala mwanamke uwe
tayari kuacha kazi kwa ajili ya kuzuiwa kuwa katika stara, kwani rizki anatoa
Allah.
Wakati naanza kazi ya udereva, nilitakiwa
na Askari wa barabarani kuvua Nikabu kwa maelezo kuwa haifai kuendesha chombo
cha moto nikiwa nimevaa vazi hilo. Hata hivyo niliwaeleza kuwa nipo tayari
kuacha kazi, lakini sio kuvua vazi hijab. Mungu alikuwa name ninaendelea na
biashara hii mpaka leo.
Pia nimepata changamoto kutoka
kwa abiria, wengi walikuwa wakiikwepa Bajaji yake wakihofia uvaaji wake,
wengine wakimfanyia kila aina ya kebehi.
Lakini nilibakia na msimamo wangu
na walio panda aliwapa huduma yake vizuri na kupata riziki yake na kadri siku
zilivyozidi kwenda, abiria walijenga imani naye na kwa sasa amekuwa na wateja
wengi wakipanda chombo chake bila hofu kwa kuwa wameshamzoea.
Mafanikio yake…
Namshukuru Mungu kupitia kazi hii
mpaka sasa naweza kumsomesha mwanangu na kumiliki kiwanja ambapo tamaa na
malengo yangu ni kujenga nyumba ya kisasa.
Sio vibaya kama Waislamu wataniunga
mkono kwa kunisadia vifaa vya ujenzi kama vile matofali, sementi na mbao. Bi.
Fatuma, anapatikana kupitia namba za simu:-0719 319 348.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni