Zinazobamba

NGOME YA MAMA SAMIA KAWE KUFANYA KONGAMANO LA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.

*Lengo ni kuunga mkono jitihada za Dkt.Samia kutangaza matumizi ya Nishati safi y kupikia.

Na Mussa Augustine.

Kikundi Cha Wamachinga"Ngome ya mama Samia"Kawe ,Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na kampuni ya Camgas -Camel Oil Ltd,kimeamdaa kongamano la kuhamasisha Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia litakalofanyika Msasani Beach  August, 26 Mwaka huu. 

Kongamano hilo litakua na fursa mbalimbali ikiwemo kutoa Elimu juu ya matumizi sahihi ya gesi safi ya kupikia ili jamii iweze kuachana na matumizi ya Nishati chafu ikiwemo kuni na mkaa ambayo imekua ikiathiri afya za watumiaji pamoja Mazingira kwa ujumla.

Taarifa hiyo imetolewa leo August 21,2025,katika Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es salaam na Mratibu Mkuu wa Kongamano hilo Potipoti Ndanga wakati akizungumza na Waandishi wa habari nakusema kuwa kufanyika kwa kongamano hilo ni kutokana na utafiti walioufanya kuanzia ngazi ya Serikali ya mtaa,huku kaulimbiu yake ikiwa ni"Gesi safi ni habari ya Mjini".
"Nawaomba wakazi wa Wilaya ya Kinondoni kupitia Majimbo yake ya Kawe,Kinondoni ambapo jumla ya kata 20,tumefanya utafiti kuanzia ngazi ya chini(grassroot)ambapo kwa wenye viti wa Serikali za mtaa tumefanya utafiti tukapata mpishi bora mmoja kwenye kata ambaye kuwakilisha kata katika Mashindano ya kumpata mpishi bora kwenye kongamano hilo."amesema Ndanga 

Nakuongeza kuwa "Tumewapata wakina mama na kutoka kata 20,ambao watakuja kwenye Mashindano ambayo Jimbo la Kawe ni kata 10 na Kinondoni ni kata 10.

Aidha Ndanga amesema kuwa lengo ni kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amekua kinara katika kutangaza Nishati Safi ya kupikia,sasa kama Rais wa Nchi anatumia Gesi safi ya kupikia,kwanini wewe Mwananchi tunaenda wapi,tunafanya nini tusitumie gesi safi ya kupikia? 
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni,Mtendaji wa Kata ya Kawe  Husna Nondo amesema kuwa kutumia Nishati safi ya kupikia inasaidia kuweka  Mazingira Safi katika Manispaa hiyo.
"Tunataka kata zetu zote 20 za Manispaa ya Kinondoni,ikiwemo kata ya Kawe Mitaa,na wafanyabiashara waweze kutumia Nishati safi ya know,na siku ya kongamano tutatoa Elimu mbalimbali juu ya matumizi bora ya Nishati Safi kwa ajili ya kumuunga mkono Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan"

Aidha amesema kuwa nishati safi imewafikia Wananchi wa kata ya Kawe,na hivyo Wananchi wawe tayari kuhamasisha  kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Nae Meneja Mkuu wa Kampuni ya Camgas-Camel Oil Ltd ambao ni wadhamini wa kongamano hilo Sadiq Abrt amesema kuwa yeye kama mwekezaji mzawa ameamua kudhamini  Kongamano hilo ikiwa ni kuunga mkono Serikali kutangaza agenda ya kitaifa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.

"Sisi CAMGAS tunatambua jitihada za Serikali,hivyo siku ya Kongamano tutatoa punguzo kwa Wananchi watakaonunua mitungi ya gesi ya kupikia  ili kuhakikisha jamii inatumia nishati hii muhimu ambayo haiathiri afya na Mazingira ya Wananchi" amesema.
Kwa upande wake Balozi namba moja wa kampuni ya CAMGAS-CAMEL OIL LTD  Dotto Magari amewahamasisha Wananchi wa Kinondoni kuachana na matumizi ya nishati chafu ya kupikia na badala yake watumie nishati safi ikiwemo Gas itokanayo na kampuni ya Camgas.

Vileve Vlezi mlezi wa kikundi cha ngome ya Mama Samia( Wamachinga)Kawe, Zainabu Athuman Janguo amesema kuwa ngome hiyo ina wanachama wapatao 459,nakusisitiza kwamba wataendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Dkt.Samia katika kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya kupikia.
"Tutalizindua kongamano hili kwa mara ya kwanza katika Wilaya ya Kinondoni maeneo ya "Msasani Beach"siku ya terehe 26 mwezi huu,lakini tunampamgo wa kufanya kongamano hili katika Halmashauri zote za Mkoa wote wa Dar se salaam,pia tutakua na mashindano ya kutafuta mpishi bora ambaye atapatiwa zawadi ya  jiko la gas safi ya kupikia" amesema Janguo.



No comments