Bashungwa kufungua Taifa CUP leo, Wasanii lukuki kuchagiza
Na.
John Mapepele
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Innocent Bashungwa (Mb) leo Desemba
10, 2021 anazindua Mashindano ya Taifa CUP 2021 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini
Dar es Salaam.
Mhe.
Bashungwa amesema Serikali imeamua kufufua mashindano hayo ili kupata vipaji vya
wachezaji ambavyo vitaendelezwa ili Tanzania iweze kufanya vizuri zaidi katika
mashindano ya kimataifa.
“Lengo
la mashindano hayo pia ni kuwashirikisha wanamichezo kutoka mikoa yote ya Tanzania
bara na visiwani.Tunatarajia yatasaidia
kuleta umoja na mshikamano, kutoa ajira na kuimarisha afya za wachezaji wetu.
Amemshukuru
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia
kurejesha mashindano hayo ambayo yalikuwa yamesimama kwa miaka kadhaa.
Aidha,
amesema mashindano ya mwaka huu yameboreshwa
tofauti na yale ya awali ambapo amesema maboresho hayo ni pamoja na
kuingiza michezo mitatu; soka kwa wanaume na wanawake, netiboli na riadha kwa
wanaume na wanawake ambapo awali ulikuwa mchezo mmoja tu wa soka.
Pia
amesema mashindano haya yameshirikisha pande zote mbili za Tanzania ili kuwa na
sura ya kitaifa
Katibu
Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi amesema uzinduzi huo
utapambwa burudani kutoka kwa wasanii wa kizazi kipya, michezo ya jadi na Bendi
ya Muziki.
Amewataja
wasanii wataotumbuiza kwenye uzinduzi huo kuwa
ni pamoja na Dulla Makabila, Isha Mashauzi, Fid Q, Madee, Lucy Charles, Bahati
Bendi na kikundi cha hamasa cha michezo ya jadi.
Aidha,
Dkt. Abbasi amesema kuwa mechi ya mpira wa Miguu ya wanaume kwa ajili ya ufunguzi
rasmi wa mashindano hayo itakuwa baina ya timu ya Kaskazini Unguja na Timu ya
Mkoa wa Mtwara.
Mhe.
Bashungwa, ametoa rai kwa vyama vya michezo na mashirikisho kuja kwenye mashindano
hayo ili kuona vipaji vya wachezaji ambao wanaweza kuwachukua kwenye vilabu
vyao.
Pia
amefafanua kwamba tayari Wizara yake imeandaa mkakati wa michezo ambao
umeainisha michezo ya kipaumbele. Michezo ya kipaumbele inajumuisha Soka,
Riadha, Ngumi, Mpira wa Wavu, Mpira wa Kikapu na Mpira wa Pete (Netiboli).
Hakuna maoni
Chapisha Maoni