WANANCHI WAMETAKIWA KUTOFUMBIA MACHO NA KUTOA TAARIFA ZA VITENDO VYA UKATILI VINAVYOFANYIKA KATIKA JAMII
Wanaharakati na wananchi kote nchini wametakiwa kuhakikisha wanachukua hatua za haraka sana endapo wanakutana na matukio ya ukatili ili kuweza kupunguza tatizo hilo na kuondokana na dhana ya kila jambo kuisubiri serikali ifanye.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP. Lilian Liundi akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mbele ya wanajamii kutoka kata mbalimbali za jiji la Dar es salaam. |
Wito huo
umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP. Lilian Liundi katika semina za Jinisia
na Maendeleo (GDSS) zinazofanywa na shirika hilo kila siku ya jumatano makao
makuu ya shirika hilo Mabibo jijini Dar es salaam.
Aidha amesema
kuwa tunapotoka katika maeneo yetu kuna ukatili mwingi na mkubwa, hivyo ni lazima
tusema na tuchukue hatua ili kuweza kusaidiana kutokomea ukatili huu.
Ameongeza kwa
kusema kuwa tunapoangalia masuala ya ukatili inabidi tuyaangalie kwa upana Zaidi
kwani kuna makundi ambayo yanafanyiwa ukatili mkubwa sana na hayana fursa ya
kujitetea kama watu wenye ulemavu.
“Lakini pia
napenda kuwakaribisha watu mbalimbali wanajamii, wanafunzi wa kada zote kuweza
kufanya kazi na Mtandao wa Jinisia Tanzania(TGNP), ili tuweze kusaidiana kuleta
vuguvugu la ukombozi wa wanawake kijinsia” amesema Lilian Liundi
Kwa upande
wake mshiriki wa semina hiyo Rebeca Rebby ambaye pia ni mzazi na mmiliki wa kituo
cha Watoto wenye usonji, ameitaka jamii kutofurahia ukatili mbalimbali wanaofanyiwa
Watoto wenye ulemavu hasa wenye usonji kwa kuwa ukatili huo unaathiri Maisha yao kwa
kiasi kikubwa sana.
Ameendelea kusema
kuwa wanaharakati nao wanatakiwa kupaza sauti ili kuweza kutokomeza vitendo
hivyo na pia ametoa Ushuuda wa mtoto mwenye usonji ambaye amebakwa na
kulawitiwa kwa Zaidi ya miaka tisa.
“Mimi kwenye kituo changu nini mtoto aliyefanyiwa ukatili wa kubakwa na kulawitiwa akiwa na miaka tisa na mpaka sasa ana umri wa miaka 16, na pale alipokuwa anaishi majirani walijua hilo lakini walishidwa hata kutoa taarifa mpaka mtoto ameharibika, Na polisi wameikataa kesi kwa kusema mtoto mwenye usonji hawezi kumbaini mtu aliyembaka hali iliyofanya watuhumiwa kuachuwa huru” amesema Rebeca
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Kipunguni Bi. Fatma Adulahmani akitoa wasilisho la namna wanavyofanya kazi katika kata yao. |
Naye mwenyekiti
wa kituo cha taarifa na maarifa Kipunguni Bi. Fatma Abdallahmani amesema kuwa
wao kama kituo wamekuwa wakiwakomboa wasichana mbalimbali katika kata yao ili
wasikeketwe na kuweza kuwapa mafunzo mbalimbali ya kujikwamua kiuchumi.
Ameongeza pia wamekuwa wakiwapa elimu mbalimbali wazee wa kimila ambao ndio wanafanya kazi ya kukeketa watoto pamoja na wazazi wanaotaka kukeketa Watoto wao, ili waachana na kazi hiyo na kuamua kuingia katika ujasiriamali wa kulima mboga na kufanya shughuli nyingine za halali za kujipatia kipato.
Baadhi wa washiriki wa Semina wakifuatilia mafunzo kwa umakini mapema jana jijini Dar es salaam. |
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP. Lilian Liundi akiongea na wanajamii kutoka kata mbalimbali za jiji la Dar es salaam. |
Afisa Programu Mkuu wa TGNP. Shakira Mayumana akiongea na Wanaharakati wa kata mbalimbali za jiji la Dar es salaam. |
Washiriki wa semina wakifanya kazi za vikundi. |
Afisa wa TGNP. Anna Kikwa akiendesha mjadala katika semina za GDSS mapema jana jijinin Dar es salaam. |
Semina ikiendelea. |
Hakuna maoni
Chapisha Maoni