NSSF yajivunia kutoa elimu kwa wanachama wake Dar
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) Masha Mshomba akielezea huduma zinazotelewa na NSSF katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa. |
Mkurugenzi akifafanua jambo katika maonyesho hayo |
Wiki ya Huduma za Kifedha Kitaifa
…NSSF yajivunia kutoa elimu kwa wanachama wake
Dar
Na Isack Magesa
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
umesema umefanikiwa kutimiza malengo yake ya utoaji ya elimu kuhusu hifadhi ya
jamii, umuhimu wa kujiwekea akiba, huduma zinazotolewa kwa njia ya mtandao
pamoja na kueleza fursa za uwekezaji kwa wanachama katika Maadhimisho ya Wiki
ya Huduma za Kifedha Kitaifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa jijini humo na Mkurugenzi Mkuu
wa Mfuko huo, Masha Mshomba katika ufunguzi wa maadhimisho hayo ambapo
amebainsha kuwa kufanikiwa kutoa elimu ya umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa
wateja na watu waliohudhuria katika banda lao.
"Tumetimiza malengo yetu ya kutoa elimu
kwa wateja tumewaeleza wateja na wanachama umuhimu wa hifadhi ya jamii
inavyomsaidia mtu anapostaafu au anapokosa uwezo wa kufanya kazi.
Mkurugenzi huyo amesema wametoa elimu ya
umuhimu wa kuweka akiba kwa wanachama na wateja unavyoweza kuwasaidia siku za
baadaye hasahasa wanaposhindwa kufanya, kustaafu na majanga.
Amesisitiza kuwa mfuko huo si watu
waliopo katika sekta rasmi hivyo hata watu wasio kwenye sekta hiyo wana fursa
kujiunga na kuchangia kwani manufaa yake ni makubwa.
Amefafanua kuwa wateja na wanachama wamepewa
elimu ya kuwekeza katika maeneo mengine ikiwemo fursa ya kuwekeza katika
hatifungani hivyo wameelezwa kuchangamkia fursa hiyo.
Akifungua maadhimisho hayo Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Jamal Kassim Ali amesema Serikali
imepanga kutumia fedha kwenye mitaji ya wajasiriamali wadogowadogo ambao
wanatoa huduma za kifedha kwenye Mpango wa Maendeleo ya sekta ya Fedha hapa
nchini.
Waziri huyo amaesema elimu ijikite kwenye
huduma za Fedha ili waweze kukuza kipato cha mtu mmojamoja na kuongeza mapato
kwa taifa hivyo ni vyema kujipima ipasavyo ili kuongeza ufanisi kwenye huduma
za kifedha hapa nchini.
Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Kifedha
Kitaifa yameanza Novemba 8 na yanatarajiwa kuhitimishwa Novemba 14 mwaka huu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni