Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Gabriel anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi kwenye semina endelevu ya AQRB
Na Mussa Augustine.
Bodi ya Wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji Majenzi( AQRB) imeishauri jamii
kutumia wataalamu wa ujenzi waliosajiliwa ili kusaidia miradi ya ujenzi kudumu
kwa muda mrefu nakwamba hali hiyo
inasaidia kupunguza gharama za ujenzi .
Ushauri huo umetolewa na Mbunifu Majengo Arch.Msajiri wa
Bodi hiyo Edwini Nnunduma wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati
akitoa taarifa ya mafunzo endelevu ya CPD yatakayofanyika mkoani Mwanza Desemba
2 na 3 Mwaka huu huku Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Mhandisi Gabriel Robaert.
Arch.Nnunduma
amesema kwamba baadhi ya Jamii
imekua ikitumia mafundi waliosomea katika vyuo vya ufundi mbalimbali kama vile
VETA katika kufanya shughuli za ujenzi
bila kutumia wataalamu wa ujenzi waliosajiriwa na bodi hiyo hali ambayo amesema
inachangia majengo mengi kutokua na ubora.
“Sisi tunasisitiza wataalamu wetu watumike hata katika
kazi binafsi,inasaidia kufahamu ghamara za ujenzi kabla ujenzi hujaanza
kufanyika,lakini pia inasaidia kujenga nyumba zenye ubora kulingana na uwezo wa mtu kiuchumi”amesema ARCH.Mnunduma.
Kuhusu semina ya mafunzo endelevu Nnunduma amesema kwamba
Semina hiuo inatarajiwa kuwa na washiriki wapatao 250 hadi 300 ambao ni
wataalamu katika sekta tofauti ikiwemo Wabunifu wa Majengo,Wakadiriaji wa
Majenzi,Wasimamizi wa Majengo,Wasimamizi wa Miradi na Wasamabazaji wa Vifaa vya
Ujenzi.
Aidha amesema kuwa mada mbalimbali zitajadiliwa ,ikiwemo
mada kuhusu sheria mpya ya Kodi kwenye Sekta ya Ujenzi ambapo wataalamu hao
watafundishwa namna ya kupeleka mapato TRA kwa njia ya kielektroniki kutokana
na mabadiliko ya kiteknolojia na kisayansi.
Kwa upande wake Msajili Msaidizi wa Usajili na Mafunzo wa Bodi hiyo Bundala
Mashaka Robaert amewaomba washiriki wajitokeze kwa wingi kushiriki semina hiyo
waweze kujengewa uelewa kuhusu mabadiliko ya teknolojia yaliyopo kwa sasa.
“Washiriki wajitokeze kwa wingi,makampuni binafsi
yawawezeshe wataalamu waweze kushiriki semina hii ni muhimu sana manake mada
ambazo tunaenda kuzijadili zitatusaidia sana katika utendaji wetu wa kazi ,pia
semina hii hufanyika mara mbili tu kwa mwaka “amesema Msajili huyo Msaidizi
Hakuna maoni
Chapisha Maoni