WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA KATIKA SOKO KUU LA AFRIKA.
Wanawake na vijana wametakiwa kuamka na kuchangamkia fursa zipatikanazo katika soko Huru la Afrika kwa kuwa wabunifu na kufanya utafiti wa bidhaa zinazohitajika kwa wingi katika soko hilo.
Muwakilishi wa nchi katika Bunge la vijana la dunia Mansouza Kingu akiongea na wanasemina za jinsia na maendeleo(GDSS) jijini Dar es salaam. |
Hayo
yameelezwa mapema wiki hii na Muwakilishi wa nchi katika Bunge la vijana la
dunia Mansouza Kingu katika mfurulizo wa semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS)
zinazofanyika kila jumatano makao makuu ya TGNP Mabibo jijini Dar es salaam.
Aidha Mansouza
amewaambia kuwa fursa moja wapo ya soko hili ni kuondolewa kwa vizuizi
mbalimbali vya kibiashara baina ya taifa moja na jingine barani afrika.
Na pia kwa
hapo baadae itakuwa na kuvuka mipaka bila passport kwa mataifa ya ndani ya bara
la Afrika kama Agenda ya Umoja wa Afrika ya mwaka 2063 ya afrika tuitakayo inayotaka
Afrika iwe moja na vizuizi vyote viondolewe.
Ameendelea kusema
kwamba mpaka sasa nchi zilizokubali kusaini makubaliano hayo ni nchi 54 za
barani Afrika na nchi 41 mpaka sasa zimeshaanza kulasimisha hili zoezi Tanzania
ikiwemo.
“Na hii inatupa picha ya kwamba muamko umekuwa
ni mkubwa sana hivyo sisi kama Watanzania tunatakiwa kuchangamka ili
tusiwatengenezee mazingira wenzetu waje kunufaika kupitia sisi” amesema Mansouza
“Soko kuu la
afrika linaenda kuwa soko kubwa Zaidi duniani toka kuanzishwa shirika la
biashara duniani yaani (WTO) Word Trade Organization, lakini pia soko hili
litakuza biashara ya afrika kwa asilimia 50 na hii ni faida kubwa kwa bara lote
la afrika”. Amesisitiza Mansouza
Ameongeza
kuwa kwa uwepo wa soko hili endapo litakamilika kwa kila kitu katika
utekelezaji wake inakadiliwa kuwa DDP ya afrika itapanda kwa Billion 3.5 za
kimarekani na kusaidia kukua kwa uchumi wa dunia kwa kiwango cha dola 75
milioni za kimarekani.
Na mwisho
ameongeza kuwa elimu Zaidi inabidi itolewe kwa jamii, serikali na mashirika
binafsi waweze kuwaelimisha wananchi namna ya kunufaika na soko hili kwani bila
elimu watu wengi hawatajua kama kuna kitu cha aina hii na matokeo yake yatanufaika
makundi machache yenye taarifa sahihi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni