Zinazobamba

MIKOPO YA HALMASHAURI IMEKUWA NI KIKWAZO KIKUBWA KWA WANAWAKE KUWEZA KUFIKIA NDOTO ZAO.

Afisa wa TGNP Flora Kamamy akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mbele ya washiriki wa semina.

Imebainika kuwa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri mbalimbali hapa nchini imekuwa na changamoto nyingi zinazosababisha watu kushindwa kupata mikopo hiyo na hata wanaopata wanapata kwa masharti mengi yasiyo rasmi.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wakazi wa mkoa wa Dar es salaam waliposhiriki katika semina za jinisia na maendeleo(GDSS) zinazoendeshwa na shirika lisilo la kiserikali la TGNP kila siku ya jumaa tano saa tisa alasiri.

Katika semina hiyo iliyofanyika mapema jana octoba 20, 2021 Makao makuu ya shirika hilo Mabibo jijini Dar es salaam, Ambapo mada kuu ilikuwa ikisema uwezeshaji wanawake kiuchumi Tanzania zipi fursa na vikwazo?

Na hapo ndipo washiriki wengi wakaamka kwa kuanza kuilaumu mikopo inayotolewa na halmashauri mbalimbali nchini kwakuonekana zimekuwa ni kikwazo kikubwa kwa wanawake na watu wengine kwa ujumla.

Kwa upande wake mshiriki wa semina kutoka kata ya mabibo Mteganda Hossein amesema kuwa kwa upande wa mikopo ya halmashauri uwa inatoka kwa ulasimu mkubwa sana kwani wanasiasa wanaona ndio sehemu ya wao kujipatia kura na wanatoa kwa watu wa chama kinachoshinda ucchaguzi husika.

Ameongeza pia kwa upande wa taasisi nyingi endepo mwanamke anahitaji msaada wa kifedha na kikubwa kinachotakiwa ni kuwa na andiko nayo ni sababu kubwa inayowakwamisha wanawake wengikatika kufikia malengo yao kwani walio wengi hawajui hata kusoma hayo maandiko watayaandika vipi?

Naye Zinabu Mmari amesema kuwa ile mikopo ya 4, 4, 2 imekuwa na changamoto kubwa kwani kwani wanaopewa mikopo hiyo hawana elimu sahii ya matumizi ya mikopo hiyo na ndio maana wanachukua baadae inapotea bila manufaa yoyote na wanawake hao pamoja na vijana na walemavu wanashindwa kupeleka marejesho.

Ameongeza kuwa baadhi ya wahusika wa kutoa mikopo hiyo wamekuwa ni watu wanaohitaji chochote kitu ili uweze kupitishiwa katiba yako, kwani hata ukienda na katiba nzuri utazngushwa kwa lengo la kuhitaji ununue katika ya kwao na wao wapate fedha pia.

aidha ameendelea kusisitiza kuwa changamoto nyingine ni kuwa watu mnakuwa wengi kwenye kikundi labda kumi alafu pesa mnapewa kidogo lakini inakuwa na masharti mengi ambayo mengine siyo rasmi kama kuna wengine wanaambiwa mwenyekikundi aende na hati ya nyumba itakayotumika kama dhamana.

Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzo kwa umakini.

Dada Josephine Jonathan Mshiriki kutoka Mbezi akiwasilisha kile walichokijadili katika kundi lao.

Mshiriki wa semina za GDSS kutoka kata ya Mburahati Roda Mdoe akilelezea jambo wakati wa kuwasilisha kazi za vikundi.

Mshiriki wa semina kutoka kata ya Mabibo Mteganda  Hussein akitoa wasilisho la kile walichokijadili katika kundi lao.

Washiriki wakiwa katika kazi za vikundi.
Washiriki wa semina wakifuatilia kinachofundishwa katika semina za GDSS.

Washiriki wakijadiliana katika kazi za vikundi.

Mzee Hamisi Masanja Katumwa akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mbele ya washiriki wa semina ambao hawapo pichani.

Semina ikiendelea.

Hakuna maoni