Zinazobamba

Makampuni ya Uwekezaji kutoka Jamhuri ya Cheki yawasili Nchini.

Na Mussa Augustine.

Naibu waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Cheki Ing.Miloslav Stasek amewasili hapa nchini akiwa ameambatana na baadhi ya wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchini humo ikiwa ni ziara ya kuangalia fursa za uwekezaji hapa nchini Tanzania.

Akizungumza jijini Dar es salaam  katika mkutano na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC )Dr.Maduhu Kazi amesema kwamba ujumbe huo umekuja ikiwa ni jitihada zilizofanywa na balozi wa Tanzania Nchini Ujerumani Dr.Abdalah Possi ambaye amekua akishawishi makampuni makubwa kuja kuwekeza hapa nchini.

Dr.Kazi amesema kwamba wawekezaji hao kutoka Jamhuri ya Cheki wameonyesha nia yakuwekeza katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuongeza thamani ya  mazao ya kilimo kama vile Pamba,Viwanda vya Nguo,Kuwekeza kiwanda cha Kutengeneza  Ndege,pamoja na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo hususani katika viwanda vya mafuta ya kula,

"Leo tumepokea ujumbe  mzuri kutoka Jamhuri ya Cheki,tumezungumza mambo mengi tunaamini tutafanya vizuri katika uwekezaji na biashara,TIC baada ya kufanya taratibu zote tunaamini tutapata wawekezaji wazuri na wenye manufaa makubwa kwa nchi yetu" Dr.Maduhu amewambia hayo waandishi wa habari.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Cheki  Miloslav Stasek amesema kwamba mazungumzo yao na TIC yamekua ya mafanikio makubwa nakwamba Makampuni Makubwa yameonyesha nia yakuja kuwekeza katika maeneo mbalimbali ikiwemo Viwanda vya teknklojia za kilimo,pamoja na kuzalisha vifaa tiba kwa ajili ya  kukabiliana na Uviko 19. 

" Tanzania ina fursa nyingi za uchumi,hivyo tumekuja kuangalia mazingira ya uwekezaji tutashirikiana vyema na serikali  kupitia Wizara ya Biashara na Viwanda katika kuhakikisha makampuni yetu makubwa yanakuja kuwekeza" amesema Ing. Stasek.

Nae Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dr. Abdalah Possi amesema kwamba huu ni wakati wa wafanyabiashara wa Kitanzania kuchangamkia fursa ya kuingia ubia na makampuni ya kigeni katika kufanya biashara na kuwekeza kwenye sekta mbalimbali nakuweza kukuza sekta ya viwanda na uchumi kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Dr. Possi takribani Makampuni Makubwa Matano ya Jamhuri ya Cheki  yamekuja kuangalia mazingira ya uwekezaji ikiwemo kampuni kubwa ambayo ina nia yakuwekeza kiwanda cha kutengeneza Ndege ndogo ambazo zinaweza kuhusika kwa Jamii pamoja na biashara kwa Ujumla,nakwamba kuna makampuni mengine makubwa yanania yakuja kuwekeza.

Hakuna maoni