Zinazobamba

Makumbusho Ya Taifa Yadhimisha Kumukumbu Ya Miaka 22 Ya Kifo Cha Hayati Mwalimu Nyerere, Yatoa Wito Kwa Jamii Kumuenzi Kwa Vitendo.

Na Mussa Augustine.

Katika kuadhimisha siku ya Kumbukumbu ya miaka 22 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Makumbusho ya TaifaJijinini Dar es salaam, imewakutanisha wanafunzi kutoka shule  mbalimbali kwa ajili ya kujifunza vielelezo vya kazi mbalimbali alizokua akizifanya mwalimu Nyerere enzi ya uhai wake.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Bw. Achiles Bufure amesema  wameamua kufanya maonyesho hayo kwa wanafunzi kwa lengo la kuwafundisha watoto uzalendo ambao Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alikua akipigania nakuwafanya watanzania kua na mshikamano.

"Mwaka huu tumeamua kuazimisha kitofauti, tumeandaa maonyesho ambayo yanaonyesha mwalimu alikua  Mkoani Lindi akihamasisha wananchi kujiunga na Chama cha TANU huku akijificha kwenye nyumba nakutumia baiskeli nanpikipiki ili wakoloni wasimuone, kwahiyo watu wengi wanajua alikomea Dar es salaam maeneo ya Pugu na Magomeni  pekee, lakini Kumbe alitembea na Mikoa mingine ikiwemo Lindi na Mtwara" amesema Bufure.

Amesema kwamba makumbusho ya Taifa inajukumu kubwa la kujenga uelewa wa uzalendo  kwa jamii kuanzia ngazi ya watoto na watu wazima, hivyo ameitaka jamii kuendelea kujitokeza kutembelea makumbusho ya Taifa ili wajifunze mambo mbalimbali kutokana na kuwekwa kwa gharama ndogo za kutembelea makumbusho hayo.

Kwa upande wake Afisa Elimu Mwandamizi Makumbusho ya Taifa Bi. Anamery Bagenyi amesema  kwamba Makumbusho ya Taifa imekua na utamaduni wakuwalika wanafunzi kwa ajili yakujifunza kwa vitendo uzalendo kwa Taifa lao wakiwa bado na umri mdogo, nakwamba hiyo ni kumuenzi Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere ambaye alikua akisisitiza uzalendo , mshikamano nakufanya kazi kwa bidii  enzi ya uhai wake.

"Hapa tunatarajia wanafunzi zaidi ya elfu moja kutoka shule ambazo tumezipa mwaliko wakuleta watoto kujifunza ikiwemo shule ya sekondari  St.Matthew's, Shule ya Msingi Umoja, Shule ya Msingi Osterbey na zingine, hii ni hatua nzuri sana kutoa elimu kwani tumekua tukitoa elimu pia kwa wananchi wengi  kupitia waimbaji wa muziki pamoja na vikundi vingine mbalimbali" amesema  Bi Anamery.

Hata hivyo Mwalimu wa Shule ya Sekondari St. Matthew's, Bw. Emanuel Lukuwi amesema sifa zilizopo za Mwalimu Nyerere nivizuri  jamii isiishie kuzisema peke yake bali iweze  kuziishi katika maisha yao ya kila siku ,akitolea mfano uzalendo ambapo amewaomba watanzania kuendelea kua wazalendo kwa vitendo.


Lethisia Julius na Bleiz Nchia wanafunzi kutoka  Shule ya sekondari St. Mathew's wamesema kwa nyakati tofauti kuwa wanamkumbuka Mwalimu Nyerere kama kiongozi ambaye alikuwa Mstari wa Mbele kukemea ukabila,udini na kuhamasisha na umoja na mshikamano.


Kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere huadhimishwa Oktoba 14 kila mwaka ambapo mwaka huu kitaifa inafanyika Wilayani Chato Mkoani Geita ambapo inaenda sambamba na zoezi la uzimaji wa Mwenge wa Uhuru.

Hakuna maoni