Zinazobamba

WANAGDSS WATAKA MWANAMKE WA KIJIJINI APEWE HAKI YAKE STAHIKI KAMA BINADAMU MWINGINE.

Kuelekea siku ya wanawake wa vijijini ambayo uadhimishwa kila ifikapo tarehe 15 mwezi oktoba kila mwaka, washiriki wa Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) wamekutana lengo likiwa ni kujadili changamoto anazokumbana nazo mwanamke wa kijijini na namna ya kuzitafutia ufumbuzi.

Mwanachama wa TGNP, Bi, Rehema Mwateba akielezea jambo katika semina za GDSS.

Akiongoza semina hiyo Mwanachama wa TGNP, Bi. Rehema Mwateba amesema kuwa wanawake wa vijijini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi katika maisha yao ya kila siku, kwani wao ndio walezi wa familia lakini pia wanajukumu kubwa la kulisha nchi kwa kuwa wao ndio wengi waliopo katika sekta ya kilimo kuliko hata wanaume.

Ameongeza kuwa pamoja na mwanamke wa Kijiji ndiye mzalishaji mkubwa wa chakula kinachotumiwa na taifa zima lakini amekuwa akinyimwa haki yake anayostahili kama kushirikishwa katika vikao vya maamuzi, kunyimwa haki ya kumiliki ardhi ambayo ndio nyenzo kubwa ya uzalishaji wake.

Ameendelea kusisitiza kuwa mashirika mengi yanayotetea haki za wanawake yanataka wanawake waweze kushiriki katika nafasi za  maamuzi kwa kuwa wao ndio wanaokutana na hizi changamoto moja kwa moja hususani wanawake wa vijijini, kwani wao ndio wanaoenda umbali mrefu kutafuta maji, lakini wakilima kufikisha mazao yao sokoni inakuwa ni shida pamoja na umbali wa zahanati wakati wa kujifungua.

Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wamesema elimu ya kutosha ikitolewa itawasaidia wanawake hao wa vijijini kwani wataweza kujitambua na kufahamu jinsi gani wanapaswa kupigania na kusimamia haki zao.

Washiriki wakifuatilia mafunzo kwa umakini.
Kwa upande wake mshiriki wa semina hiyo Bi Zuwena Juma anasema niwakati wa kumtua mzigo mwanamke wa kijijini ili nae aishi kama mwanamke wa mjini ili aweze kufurahia maisha na kuendelea kuzalisha kwa wingi na taifa linufaike kwa kupata mapato kupitia kodi.

Ameongeza kuwa mwanamke wa kijijini nae aweze kushirikishwa katika maamuzi mbalimbali hasa ya kiuchumi na siyo anaonekana bora kwenye kuzalisha lakini kuuza mazao anauza mwanaume na pesa anapokea yeye peke yake, lakini pia aweze kusogezewa karibu huduma za kijamii kama Maji, Shule pamoja na Huduma za afya.
Mwanachama wa TGNP, Bi, Rehema Mwateba akielezea jambo katika semina za GDSS.
Washiriki wa semina wakifuatilia mafunzo kwa umakini.
Washiriki wa semina wakiwa katika kazi ya kikundi.
Semina ikiendelea.

Washiriki wakijadili katika kazi ya kikundi.

Hakuna maoni