Zinazobamba

TBBF yawataka washiriki shindano la Mr Tanzania kufuatilia kwa umakini.

 Na Mwandishi Wetu.

Washiriki wa Shindano la Mr.Tanzania wameatakiwa kujifunza mikakati ya shindano lenyewe kama vile anuwai zilizotajwa kutoka kwenye picha na video zilizochapishwa na video zilizochapishwa kwenye akaunti ya Instagram, Facebook, YouTube.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Shirikisho la Tanzania Bodybuilding (TBBF) Francis Mapugilo leo ambapo amesema Kwa walio tayari watalipa TSH.100, 000 kwaajili ya kujiunga kwenye shindano.

Amesema kiasi hicho hakirejeshwi ikiwa mshindani hatastahiki kuhukumu kabla, huku umri wa kushiriki ukitajwa kuwa ni miaka 18 hadi miaka 65. “Kuna aina tatu kulingana na uzito katika kitengo cha Mr. Tanzania , kila mshiriki ataingia katika kitengo kimoja , mshiriki anahitaji kuondoa uamuzi wa kabla ya kuingia kwenye shindano la mwisho,”amesema Mapugilo.

Mapugilo amesema kua ili kujisajili mshiriki anaweza kuingia kwenye wavuti yao www .tzbbf.org ambapo ataweza. Kuipakua bure. Katibu huyo ameendelea kufanya kuwa washiriki wanaoshindwa kufuata sheria wataweza kuondolewa na kuzuiliwa kwa kuonekana kwenye bmashindano ya Sasa na yale yajayo.

“Mshindi wa 1 atachaguliwa kutokana na aina 3 zote za uzani Tsh.5m , mshindi wa 2 atachaguliwa kutokana na aina 3 zote za uzani Tsh.3m huku mshindi wa 3atachaguliwa kutokana na aina zote 3 za uzani wa Tsh.1m,” amesema Mapugilo.

Kamati ya mashindano ya MR Tanzania imetaja kufanyika shindano lake October 22 mwaka huu , washiriki wote wa Mr . Tanzania watatakiwa kuripoti katika katika ukumbi wa Kilimanjaro,Ubungo Plaza Dar es Salaam siku hiyo kuanzia saa 7:00 asubuhi.

Katibu huyo amesema kuwa fomu pia zinapatikana katika kumbi za michezo mbali mbali Jijini Dar es Salaam maeneo ya Gym Bodyline Mikocheni Gym Home Mwenge, Body Fuel Masaki pamoja na Gym zingine.

Uhakika ni hivi bodybuilding safari hii itakuwa ni (Free Class) kwa maana hakutakuwa na groups kutokana na uzito wao imepambanua hivyo TBBF Wamesema kua wamefanya hivyo kutokana na ufinyu wa bajeti ya mashindano , na kutakuwa na kipengele cha best Poser ilikuleta ladha kwenye shindano.

Zawadi kwa washindi zimetajwa kuwa ni kemkem ilikuchochea amasa katika shindano hilo.

Hakuna maoni