Zinazobamba

JAMII IMETAKIWA KUACHANA NA MFUMO DUME ILI WANAWAKE WAWEZE KUZIFIKIA NAFASI ZA UONGOZI

Imeelezwa kuwa miongoni mwa vikwazo vinavyoweza kusababisha mwanamke kushindwa kufikia nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia ngazi ya chini hata juu ni mfumo dume.

Mwanaharakati wa masuala ya jinsia Bw. Deo Temba

Hayo yameelezwa na Mwanaharakati wa masuala ya jinsia Bw. Deo Temba wakati akifanya ulaghibishi katika semina ya kuwajengea uwezo Madiwani, Wenyeviti na Watendaji wa mitaa, kutoka kata ya Mabwepande, Saranga Pamoja na kata ya Ukenyenge kishapu.

Aidha muwezeshaji huyo amesema kuwa ni rahisi sana kwa mwanamke kupata nafasi kubwa ya uongozi kama Ubunge hata Urais kuliko kupata nafasi ya kuwa kiongozi katika mtaa au kata, Na hii ni kutokana na mifumo kandamizi iliyowekwa ndani ya jamii zetu kwa muda mrefu.

Ameongeza kuwa mfumo dume si kwamba ni lazima mwanaume awe akimfanyia mwanamke bali hata wanawake wanaweza kuwafanyia wanaume, lakini pia hata wanawake wanaweza kufanyiana wenyewe kwa wenyewe na hata taasisi moja kuifanyia taasisi nyingine pia inawezekana.

Ameendelea kusisitiza kitu kingine ambacho ni mawazo mgando kuwa ili wanawake waweze kuifikia hamsini kwa hamsini katika uongozi inapaswa jamii iachane na mawazo mgando kwa kuamini mwanamke awezi.

“Jamii inatakiwa kuondokana na dhana ya kwamba mwanamke ni kiumbe dhaifu, hii si kweli kwani mwanamke anaweza kufanya chochote ambacho mwanaume anafanya kama ni akili mwanamke anazo, nguvu anazo na hata uwezo anao pia, hivyo jamii inatakiwa kuachana na dhana hii potofu inayomkandamiza mwanamke kwa sabababu ya jinsi yake”.Amesema Temba

Diwani wa viti Maalum wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Mh. Liberata Samsoni akitoa ufafanuzi wa jambo fulani.

Kwa upande wake Diwani wa viti Maalum Manispaa ya Ubungo Liberata Samsoni amesema kuwa katika halmashauri ya Ubungo katika madiwani wake 19 wanawake ni 6 peke yake, huku katika wenyeviti 94 ni wanne peke yake ndio wanawake.

Ameongeza kuwa mafunzo hayo yatamsaidia kuweza kupeleka mgawanyo sawa nyumbani kwake lakini pia hata kupigania katika ngazi ya halmashauri kuwa na mgawanyo sawa wa rasilimali kwa wanawake na wanaume hususani katika matundu ya vyoo yaongezeke kwa wasichana. 

Viongozi kutoka kata ya Mabwepande, Saranga na Kishapu wakifuatilia mafunzo kwa umakini.

Afisa Programu Mkuu wa TGNP Shakira Mayumana akitoa neno katika ufunguzi wa Mafunzo ya Bajeti yenye Mlengo wa Kijinsia akimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Lilian Liundi.

Afisa Programu Mkuu wa TGNP Shakira Mayumana akiongea na washiriki wakati wa ufunguzi wa mafunzo.

Dhumuni la semina.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbopo kata ya Mabwepande Mohamed Bushiri akitoa mchango wake katika warsha ya Bajeti yenye Mlengo wa Kijinsia.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Michungwani kata ya Saranga Wiliam Frank Chitanda akieleza jambo kwa msisitizo katika mafunzo yaliyoratibiwa na TGNP.

Washiriki wa mafunzo kutoka kata ya Saranga wakipewa muongozo na muwezeshaji Bw. Deo Temba.


Diwani wa kata ya Saranga Mh. Edward Laizer akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mapema wiki hii jijini Dar es salaam.

Diwani wa kata ya Mabwepande Mh. Muhajirina Kasimu Obama akitoa ufafanuzi wa jambo katika semina iliyoandaliwa na TGNP.

washiriki wa mafunzo kutoka kata ya Mabwepande wakiwa katika kazi ya kikundi.


Hakuna maoni