Zinazobamba

Wakala wa Bima Waombwa kutoa Elimu ya Kutosha kwa Wananchi ili kufikia Malengo ya Serikali

 Na Mussa Augustine.

Kamishna wa Bima Nchini  Mussa Juma amewataka mawakala wa Bima Nchini kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu umuhimu wa Bima ili kufikia malengo ya serikali ambayo imejiwekea ya kufikia asilimia 80 ya uelewa wa Bima Kwa wananchi,pia kufikia angalau asilimia 50 ya watanzania wawe wamepata Bima mojawapo kufikia mwaka 2030.



Kamishna Mussa ametoa wito huo Dar es Salaam wakati akifungua Mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Chama Cha wakala wa Bima Nchini ambayo yamelenga kutoa elimu juu ya namma Bora ya Kuendesha uwakala wa Bima,namna yakutafuta Masoko pamoja na kufahamu mambo ya Kodi kuhusu Bima hatua ambayo itawasaidia wakala hao kufanya kazi Kwa ufanisi mkubwa.

Kamishna  huyo wa Bima kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini ( TIRA) amesema kwamba ili kufikia malengo ya serikali ni muhimu mawakala,madalali pamoja na makampuni ya Bima kuendelea kutoa elimu Kwa wateja,kuuza bidhaa za Bima kulingana na uwezo wa kampuni zao pamoja na kushughulikia na kutatua kwa haraka migogoro ya Bima inayojitokeza Kwa wateja wao.


"Kujiendeleza kielimu inasaidia kuwa nauelewa Mpana katika masuala ya Bima hususani mambo ya teknolojia na hii inawasaidia msiachwe nyuma kwenye ushindani,hivyo jitahidini Kila mmoja awe na kitu cha kipekee ili unaeshindana nae asiweze kukushinda ,kwahiyo mnapata semina hii kuwafanya msitupwe kwenye ushindani"amesema.

Nae  Mwenyekiti wa Chama Cha wakala wa Bima Nchini  Bw.Sayi Jonh Daudi ameiomba serikali kuondoa sharti la kuwekea kiwango cha fedha benki (FDR) ambacho kitatumiwa na wakala kulipa gharama za bima pindi atakapokutana na changamoto za kutenda nje ya utaratibu  kwa mteja wake nakwamba sharti hilo limekuwa kikwazo Kwa wakala wa bima ambao ni wapya.


" Tunaiomba serikali iondoe hiki kigezo  kinachomtaka mtu anaetaka kutoa huduma za bima lazima awe na kiasi Fulani cha


fedha benki ambacho kinaweza kutumika kumlipa mteja anaetendewa kinyume cha utaratibu, jambo hili limekua kikwazo kikubwa Kwa wakala wa  bima,tunaiomba ikiwezekana waiondoe " amesema Bw.Sayi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Bima ya FIDES Insuarence iliyopo Dar es salaam.
Kwa upande wao baadhi ya viongozi watendaji wa  makampuni ya wakala wa Bima akiwemo  Bi.Modesta Liviga wa Kampuni ya Primode Insuarence Agence. pamoja na Bw.Meshaki Matulile mtendaji mkuu wa Kampuni ya  BMC Insuarence Agence. wamesema Kwa nyakati tofauti kuwa Mafunzo hayo yatawasaidia kufahamu namna nzuri ya kuuza bidhaa za bima,kutafuta Masoko ya Bima hatua ambayo itasaidia kufanya kazi zao Kwa ufanisi mkubwa.

Hakuna maoni