Zinazobamba

TIC yanuia kuendelea kushirikiana vizuri na wawekezaji.

Na Mussa Augustine.
Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini ( TIC) Dr.Maduhu Kazi amesema kwamba kituo hicho kitaendelea  kushirikiana vizuri na wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nje ya nchi ili kukuza sekta ya biashara na viwanda.

Hayo ameyasema wakati akizungumza na ujumbe kutoka nchini Misri ambapo ujumbe huo umetoka katika Jumuiya ya Afro-Asia (AFASU)ambayo imeasisiwa kwa ajili ya kukabiliana na umasikini kwa kufanya biashara na uwekezaji 

Dr.Maduhu amesema kwa kuja kwa ujumbe huo nikutokana na matunda mazuri ambayo TIC ilifanya ziara Misri nakufanikiwa kuzungumza na wafanyabiashara na wawekzaji hivyo wamrkuja nchini ili kuangalia mazingira ya Tanzania nakuangali sekta muhimu za uwekezaji ikiwemo sekta ya Utalii wa fukwe.

"Sekta 16 muhimu zinatarajiwa kuwekezwa ikiwemo sekta ya Utalii,Kilimo,Elimu,Ufugaji wa Samaki,biashara na sekta zingine,hivyo ili kufanikiwa katika uwekezaji huo (TIC) inaendelea kuweka ushirikiano mzuri na wafanyabiashara wa Jumuiy hiyo." Amesema Dr.Maduhu

Awali akizungumza kiongozi wa Ujumbe huo ambaye ni raisi wa Jumuiya hiyo Dr.Hossam Darwish amesema kwamba wameamua kuja Tanzania kuangalia mazingira hususani katika sekta ya Utalii wa fukwe,pamoja na kuweza kujenga kijiji cha utalii kitakachosaidia watu kupata mapumziko na famililia zao pamoja na vyakula vya asili.

" Huu ni mwelekeo wetu mzuri kujenga kijiji fulani cha mazao ya chakula lakini pia inakua kama utalii watu wanatembelea na familia zao nakupata mapumziko na chakula cha asili,kwenye jumuiya yetu kuna wawekezajj wakubwa ambao wanaweza kufanya utalii wa aina hii" amesema Dr.Darwish.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Habari,Mawasiliano ,teknolojia ya Habari Dr.Jim Yonazi amesema kwamba kwa sasa wanaamini kwamba ujume huo utasaidi kuendeleza sekta ya viwanda nakukuza uchumi wa tanazania .

Aidha amesema kwamba wanatarajia kufanya mazungumzo pia yakukuza sekta ya tehama kwa nchi hizo mbili yaani Misri na Tanzania na kuendeleza mahusiano yakiuchumi katika uwekezaji, nakwamba masuala ya usalama mtandaoni yatapewa kipaumbele zaidi.

Hakuna maoni